Na Ahmed Mahmoud
Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara amesema Serikali imewekeza fedha nyingi sana katika sekta ya usafirishaji kwa kuongeza fursa za kibiashara nchini faida.
Aidha ni muda muafaka kwa sekta ya uchukuzi kufanya tathmini ya kina ya mwaka mzima ya fursa na faida za kibiashara ambazo serikali imekuwa ikiwekeza na kupata faida ya USD billion 13 ambayo haijawahi kufikiwa.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 16 wa wadau wa sekta ya uchukuzi kufanya tathmini ya mwaka mzima wa shughuli za sekta hiyo (16 Joint Transport Sector Review Meeting) unaoendelea kwa siku nne Jijini Arusha.
Amesema kwamba naona Kuna msongamano katika Bandari yetu ya Dar es salaam hii ni kuonyesha meli zimeongezeka sana kwa zaidi ya asilimia 30 tulikuwa tunahudumia meli 30 Hadi 60 lakini Sasa hivi tunahudumia zaidi ya meli 100.
Amebainisha hii inaonyesha hata kwa njia ya barabara mfano pale mpaka wa Tunduma kwa Takwimu za miezi mitatu zinapita takribani Tani milioni moja ya mizigo kitu ambacho hakijawahi kutokea huko nyuma,
“Sekta imekuwa sana ya usafirishaji tumekuwa tukiwaambia wadau wachukue hiyo changamoto kama ni fursa kwa sababu tunaweza kuitumia sekta ya usafirishaji kusukuma mbele maendeleo ya nchi ukiangalia sekta hii imeingiza fedha nyingi za kigeni ukitoa sekta ya madini na Utalii inayofuata ni hii”
Awali akimkaribisha kuongea na Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ufuatiliaji na tathmini wizara ya uchukuzi Devotha Gabriel amesema sekta hiyo imekuwa na mchango wa Kuingizia serikali mapato katika Pato la Taifa kwa hivi karibuni.
Hata hivyo Mkutano wetu huu ni sehemu ya kufanya tathmini ya mwaka mzima katika uendeshaji changamoto kuongeza uelewa na kujengeana uwezo kujua tulipo kuongeza weledi na uboreshaji wa sekta ya usafirishaji.