Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akizungumza na wageni kutoka nchini Korea, ugeni ambao umeongozwa na aliyekuwa mchezaji maarufu wa baseball nchini Marekani Bw. Chan Ho Park waliotembelea hospitalini hapa leo.
Dkt. Julieth Magandi akimshukuru Bw. Chan Ho Park mara baada ya kumpatia zawadi ya mpira unaotumika kuchezea mchezo wa baseball.
Bw. Park (kushoto) akimpatia mtoto zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuchezea, kulia ni Daktari Bingwa wa Watoto Dkt. Mwanaidi Amiri akifurahi baada ya mtoto kupatiwa zawadi.
Bi. Devotha Malumba akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wazazi wenzake baada ya mwanamichezo maarufu kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Mloganzila.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wa kwanza kushoto) akiagana na Bw. Park aliyetembelea hospialini hapa.
Dkt. Julieth Magandi akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka nchini Korea mara baada ya kutembelea hospitalini hapa.
…………………………
Aliyekuwa mwanamichezo mahiri wa Baseball nchini Marekani, Bw. Chan Ho Park leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kuzungumza na uongozi wa hospitali kuhusu masuala mbalimbali hususani suala la kuendelea kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Korea na Hospitali ya Mloganzila.
Bw. Park amesema anaamini uhusiano huu utaendelea kuimarishwa kwa faida ya pande zote mbili hasa katika kutoa huduma za afya.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amemshukuru Bw. Park kwa kutembelea hospitalini hapa na kueleza kuwa hospitali hii ni moja ya hospitali kubwa hapa nchini na inatoa huduma bora za afya na za kibingwa.
“Nimefurahi mmekuja kututembelea na kujionea shughuli mbalimbali za utoaji huduma zikiendelea katika hospitali yetu yenye vitanda 608,” Dkt. Magandi.
Mwanamichezo huyo ametembelea wodi ya watoto hospitalini hapa ambapo pamoja na mambo mengine amepata fursa ya kucheza na kuzungumza na watoto.