Home Mchanganyiko WAZIRI MWAKYEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 25 YA UPADRE WA...

WAZIRI MWAKYEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 25 YA UPADRE WA ASKOFU LIBERATUS SANGU

0

Na Marco Maduhu – Malunde 1 blog

Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameadhimisha miaka 25 ya Upadri tangu alipoanza utume wake mwaka 1994.

Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 ya Upadri wa Askofu Sangu imefanyika leo Alhamis Novemba 14, 2019 kwenye Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma lililopo Ngokolo Shinyanga mjini na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,viongozi wa kanisa,waumini na watu mbalimbali wenye mapenzi mema ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria maadhimisho ya Jubilee hiyo ni  aliyekuwa Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda, Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye, mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Dkt. Mwakyembe akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini kuombea amani taifa, ambalo linaelekea kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

“Serikali ya awamu ya tano inatambua mchango mkubwa wa viongozi wa dini, na ndiyo maana Rais wetu Dkt. John Magufuli kila mara amekuwa wakiomba mumuombee, ili aweze kufanikiwa katika uongozi wake na kutetea maslahi ya wanyonge, na ndiyo maana tunawaomba mzidi kuombea amani nchi yetu,”amesema Mwakyembe.

“Kwenye vipindi vya uchaguzi huwa kuna mambo mengi ambayo hutokea ya viashiria vya uvunjifu wa amani, na migogoro huwa haiwezi kukosekana, kina kinachopaswa tu ni kuomba ili uchaguzi uweze kufanyika kwa utulivu na amani,” ameongeza.

Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,Askofu Gervace Nyaisonga, akitoa salamu kwa niaba ya maaskofu wa kanisa hilo, amewataka viongozi wote wa kisiasa wakae meza moja ili kutafuta suluhu na siyo kususia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.

Aidha amewataka watanzania wajitokeze kwa wingi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa, ili wakachague viongozi bora, makini na waadilifu, ambao watawaletea maendeleo.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga,Mhashamu Liberatus Sangu amepongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya ya kuleta maendeleo hapa nchini pamoja na kupigania maslahi ya wanyonge.

Amesema kazi anayoifanya Rais Magufuli inapaswa kupongezwa na kila mtu.

“Yule ambaye atapinga maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano atakuwa na ugonjwa wa akili, na kama hana ugonjwa huo basi atakuwa ana sumbuliwa na wivu”,amesema Askofu Sangu.TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu Liberatus Sangu wa jimbo Katoliki la Shinyanga leo Alhamis Novemba 14, 2019. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,Askofu Gervace Nyaisonga akitoa salama kwa niaba ya maaskofu wa kanisa hilo, kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya updare wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

Askofu wa Jimbo la Shinyanga,Mhashamu Liberatus Sangu akitoa shukrani kwenye maadhimisho yake ya jubilee miaka 25 ya Upadri.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu. Wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, anayefuatia ni aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinga na Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamas, akiwa na mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye na nyuma yao ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao, wakiwa kwenye jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Maskofu wa majimbo mbalimbali hapa nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

Maskofu wa majimbo mbalimbali hapa nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Mapadri wa majimbo mbalimbali hapa nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Masista wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu Liberatus Sangu.

Waumini wa Kanisa la Katoliki wakiwa kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Waumini wa Kanisa Katoliki wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Waumini wa Kanisa Katoliki wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Waumini wa Kanisai Katoliki wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Wana Kwaya wa Kanisa Katoliki wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu.

Maaskofu kutoka Majimbo mbalimbali hapa nchini wakimpongeza Askofu Liberatus Sangu wa jimbo la Shinyanga kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake na kumpatia zawadi ya Fimbo ya Uaskofu.

Maaskofu wakiendelea kumpongeza Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Aliyekuwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinga akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofley Mwangulumbi, akimpongeza Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu kwa kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wake.

Awali Polycarp Kadinali Pengo akiombea Makaburi ya Maaskofu ambao walishatangulia mbele ya haki.

Muonekano wa kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Ngokolo Shinyanga Mjini mahali ambapo maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya Upadri ya Askofu wa Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu yamefanyika.

Awali maandamanoo yakifanyika ya kuingia kanisani ili kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu Liberatus Sangu.

Maandamano yakiendelea ya kuingia kanisani ili kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu Liberatus Sangu.

Maandamano yakiendelea ya kuingia kanisani ili kuadhimisha jubilee ya miaka 25 ya Upadri wa Askofu Liberatus Sangu.

Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu akiingia kanisani kuadhimisha jubilee yake ya miaka 25 ya Upadri.

Askofu wa jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu katikati akipiga picha ya pamoja na Maaskofu pamoja na viongozi wa Serikali akiwemoWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  mwenye kaunda suti pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack mwenye ushungi kichwani.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.