Mkurugenzi wa Fedha, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Pascal Karomba akiwa katika picha ya pamoja na Faustine Masalu Mhasibu Mwandamizi TASAC pamona na Bw. Nicolas Kinyariri Afisa Uhusiano kwa Umma TASAC wakiwa tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji wa Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2022.
………………………….
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kushinda tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji wa Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2022.
Utoaji wa tuzo hizo unaratibiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ulifanyika Disemba 1, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo washindi katika makundi mbalimbali walikabidhiwa tuzo zao na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Zanzibar CPA. Jamal Kassim Ally
Akizungumzia ushindi wa Tuzo hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Pascal Karomba, amesema kuwa mafanikio hayo yemetokana na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Bw. Karomba amesema kuwa siri ya ushindi wa tuzo hiyo kujituma pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma.
“Siri ya mafanikio ni ushirikiano, kutumia taaluma, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujituma katika utendaji kazi” amesema Bw. Karomba
Amesema kuwa wanaendelea na jitihada katika utendaji ili kuhakikisha mwakani wanapiga hatua ikiwemo kupata ushindi wa Jumla katika tuzo hizo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 11- 12 cha Sheria ya TASAC Na. 14 ya mwaka 2017, miongoni mwa kazi za TASAC ni kudhibiti Usimamizi wa Shughuli za Usafiri kwa Njia ya Maji, Mazingira, Usalama na Ulinzi.
Kusimamia Sheria ya meli za Biashara; Kutimiza wajibu wa kukagua meli zote za kigeni katika bandari zetu na meli zilizosajiliwa Tanzania Bara pamoja
na kuidhinisha vifaa vya huduma za usalama na watoa huduma za usafiri kwa njia ya maji.
Mkurugenzi wa Fedha, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Pascal Karomba akipokea tuzo tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji wa Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2022.
Mkurugenzi wa Fedha, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Pascal Karomba akizungumza kuhusu tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji wa Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2022.