Na Sophia Kingimali
Serikali ya Tanzania na Malawi zimesaini mkataba wa ushirikiano kuhusu ushoroba wa usafirishaji baina ya nchi hizo lengo likiwa kurahisisha usafirishaji na urahisishaji wa ufanyaji biashara
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Decemba 1,2023 jijini Dar es salaam waziri wa uchukuzi Makame Mbalawa amesema mkataba huo ni muhimu sana kwasababu Malawi wanatumia bandari ya Dar es Salaam
Amesema kwa kutumia bandari hiyo inafanya bidhaa na mambo mengine kwa Malawi bei ziwe nzuri zaidi
“Kwa vile tumeweka mkataba huo ulikuwa wa mda mrefu tumeweza kusaini upya kuhakikisha kwamba sasa unafanya vizuri zaidi”amesema Mbalawa.
Amesema Serikali imejenga miundombinu mingi kwaajili ya kuboresha ushoroba huo wa usafirishaji kati ya nchi hizo mbili
“Tumefanya maboresho makumbwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kuanzia Gate namba moja hadi namba saba pia tumejenga Gate maalum kwaajili ya gate namba zero”.amesema
Amesema kwa kuweka sekta binafsi kuwekeza kwenye bandari ya Dar es Salaam ni lengo ni kuongeza ufanisi kwenye bandari hiyo.
Akizungumzia Bandari ya Mtwara amesema wamefanya mabadiliko makubwa wamejenga gate ya kisasa mbali na urefu takribani mita 300 inafanya kazi ambapo wameweka vifaa vya kisasa.
Hata hivyo amesema wanatarajia kusaini mkataba mwingine kwa kwaajili ya ujenzi wa bandari ya Mbamba bey ambayo ni muhimu sana kwa ziwa Nyasa.
Aidha Mbalawa amesema kuwa Bandari muhimu kwaajili ya pande zote mbili hivyo jitihada zinafanywa kuhakikisha wanafungua ushoroba huo kati ya Tanzania na Malawi.
Kwa upande wa Malawi utarahisisha sana upatikanaji wa bidhaa kwa nchi yao wakitumia korido ya Mtwara itapunguza sana thamani gharama ya bidhaa na wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu
Amesema Mkataba huo waliosaini unafaida kwa Tanzania na Malawi kwani mwaka 2022 mzigo ulihudumiwa na bandari ya Dar es Salaam kwa nchi ya Malawi ulikuwa takribani ya zaidi tani laki 5 ambao ni mdogo sana hivyo wamejipanga kuhudumua mzigo mkubwa zaidi.
“Lakini ukilinganisha na mwaka 2018 kumekuwa na ongezeko kubwa hivyo tunataka ongezeko lifikie hadi tani million moja au mbili hiyo itatusaidia kuongeza ufanisi wa bandari yetu ya Dar es Salaam”ameongeza
Amesema Wamekuwa wakisaini mikataba kwaajili ya kuifungua bandari ya Dar es Salaam kwani kuna ushindani bandari hiyo wamejipanga vizuri kuhakikisha miundombinu wanayojenga sasa hakuna mtu ataweza kushindana na bandari hiyo.
Amesema Kwenye bandari ya Dar es Salaam kuna faida kubwa na fursa kwani bado hawajatumia fursa hizo zinazofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Naye Waziri wa usafirishaji Malawi Jacob Hara amesema Malawi wamefurahi kusaini mkataba huo kwani kushirikiana pamoja ni muhimu sana.
“Naamini mkataba huu tuliosaini utasaidia kufanya kazi kwa pamoja kati ya Tanzania na Malawi na kurahisisha usafirishaji ,”amesema