Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo (Wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Aliyeshika pochi) na Viongozi wengine wa Wizara hiyo walipotembelea banda la maonesho la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo wakati wa maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya viongozi, waratibu na waelimisha rika wa Wizara, Mikoa na Taasisi za Umma wakifuatilia jambo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Mjini Morogoro.