Mratibu wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma Dkt .Ezekiel Kyogo akizunungumza na Watendaji wa vikosi vya ulinzi na usalama ,Masheha na Vikundi vya ulinzi shirikishi wakati wa kongamano la kutoa elimu ya ulinzi shrikishi liliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt.Ali Muhammed Shein Mjini Unguja .
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia kongamano la kutoa elimu ya ulinzi shirikishi liliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt.Ali Muhammed Shein Mjini Unguja .
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad akizungumza na Watendaji wa vikosi vya ulinzi na usalama ,masheha na Vikundi vya ulinzi shirikishi wakati akifungua kongamano la kutoa elimu ya ulinzi shrikishi,liliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Dkt. Shein Mjini Unguja.
………
NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZ
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amewataka wananchi kujitolea kujiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuendeleza amani iliyopo Nchini.
Akizungumza wakati wa akifungua kongamano la ulinzi shirikishi huko Ukumbi wa Skuli ya Dk Ali Muhammed Shein amesema kuwepo kwa Vikundi hivyo kutasaidia kupunguza wahalifu ndani ya jamii.
Ameeleza kuwa jukumu la usalama wa Wananchi si la Jeshi la Polisi pekee hivyo uwepo wa vikundi hivyo kutasaidia kupunguza ongezeko la vitendo vya kihalifu katika jamii.
Aidha alisema kongamano hilo litaisaidia jamii iliyoshiriki kujua lengo la kuanzishwa kwa vikundi vya polisi jamii pamoja na kufanya kampeni ili jamii hiyo iweze kujiunga kusaidia vita dhidi ya vitendo viovu.
CP Hamad aliwataka Wananchi kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa ushahidi wa kesi mbali mbali zinazojitokeza katika jamii sambamba na kuwataka kutoa taarifa mapema za udhalilishaji ili kuweza kupatikana kwa ushahidi.
“Sisi jeshi la polisi tunahaki na wajibu ya kuwalinda Raia na Mali zao ila na nyinyi mna haki ya kujilinda kwa kudumisha Amani iliyopo katika jamii zetu ili tuweze kukimbiza wahalifu na tuweke usalama katika Nchi yetu.’’ Alisema
Awali alimshukuru Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaunga mkono katika kutoa ushirikiano kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili Amani izidi kuendelea Nchini.
Nae Mratibu wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma Dk Ezakiel Kyogo aliwataka wazazi na walezi kuwapa watoto mafundisho waliyokuwa wakipewa zamani ili kuzuia mporomoko wa maadili katika jamii ya Zanzibar kwa maslahi ya Taifa la kesho.
Alisema uwepo wa vikundi shirikishi katika jamii kutasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu ikiwemo uporaji, wizi,na udhaalilishaji sambamba na kuwataka wanavikundi vya polisi jamii kuandaa vipeperushi juu ya mambo ya udhalilishaji kwa jamii ili kupunguza uhalifu katika nchi yetu.
Nao Baadhi ya washiriki katika Kongamano hilo wamelishukuru jeshi la polisi kwa kuwapaatia elimu juu ya ulinzi shirikishi Sambamba na kulitaka jeshi hilo kuwa na programu maalumu kati ya jeshi la polisi, vikundi vya ulinzi shirikishi na wizara ya Elimu ili waweze kuzibiti vitendo vya uhalifu kati Taifa letu.
Kongamano hilo la siku moja liliwashirikishaWazazi ,walezi, Masheha wa Shehia zaidi ya 50,wanafunzi wa Skuli mbalimbali,Vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakijadili umuhimu wa uwepo wa Ulinzi shirikishi katika Jamii.