Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala amewatunuku vyeti wahitimu wa ngazi ya Diploma ya Ufamasia na Utabibu Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwatunuku vyeti wahitimu wa Diploma ya Ufamasia na Utabibu alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Diploma ya Ufamasia na Utabibu wakiwa katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akinutunukiwa Tuzo na Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala ya kutambua mchango wake katika elimu, wakati wa mahafali ya chuo hicho Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipata maelezo ya mfano wa utabibu kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala alipokuwa mgeni rasmi Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Afya na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa na wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa chuo Bw. Shaban Mwanga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila wakifuatilia mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala katika Diploma ya Ufamasia na Utabibu Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
…………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa wahitimu wa afya kuwa na upendo kwa watakaowahudumia pindi wapatapo fursa za kazi.
Dkt. Jafo ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala amewatunuku vyeti wahitimu wa ngazi ya Diploma ya Ufamasia na Utabibu Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wahitimu hao amewapongeza kwa kufanya vizuri katika masomo yao na kuwataka kuwa na upendo na watakaowahudumia pindi wafanyapo kazi.
Pia, amesema watoa huduma za afya ni watu muhimu sana katika taifa na ndio maana Serikali imeendelea kutoa ajira kwa kada hiyo.
Amesema kutokana na umuhinu huo Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa zahanati na hospitali ili kusogeza mbele huduma.
Amewataka wanafunzi wanaoendelea na masomo katika chuo hicho kujituma zaidi ili wanapohitimu kuwepo na wahitimu wazuri wenye kuhitajika na taifa.
Ametumia nafasi hiyo pia kuwaasa watuunze mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na athari za kimazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Bw. Shaban Mwanga amesema City College itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika sekta ya afya kwa kutoa wahitimu bora.
Ameongeza kuwa katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 60 wametunukiwa vyeti ambapo kati yao 18 wa fani ya Ufamasia na 42 wa Utabibu.
Mahafali hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila