Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF Tanzania, Elka Wisch akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha .
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Arusha .
Baadhi ya watoto wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha .
………………………….
Julieth Laizer ,Arusha
Arusha .Serikali ya Tanzania Kupitia Wizara ya ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira imezitaka taasisi za umma na binafsi pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha ulinzi wa mtoto unaendana na mabadiliko ya tabia nchi kwani mabadiliko hayo yamekuwa yakiathiri kwa kiasi kikubwa usalama wa mtoto kutokana madhara yanayoambatana nayo ikiwemo Suala la Ukame.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira, Selemani Jafo katika maadhimisho ya Siku ya watoto duniani kitaifa ambayo imeazimishwa mkoani Arusha .
Waziri Jafo amesema kuwa hali ya ukame ambayo hupelekea njaa pamoja na kukatika kwa umeme mara kwa mara huathiri kwa kiasi kikubwa Maendeleo na ustawi wa watoto.
“Upatikanaji wa haki za watoto ni jambo la msingi kwani serikali ya Tanzania imeamua kuwekeza na kuwasaidia watoto katika sekta zote na kuhakikisha wanaondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili”amesema.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa shirika la UNICEF Tanzania, Elka Wisch amesema kuwa watahakikisha kuwa wanakuwa wanawalinda watoto dhidi ya aina zozote za ukatili na pindi ukatili unapotokea wahusika wanachukuliwa hatua za haraka .
“Tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha haki za watoto zinalindwa kwani swala la kulinda haki hizo ni swala letu sote na sio kuwaachia watu fulani kufanya hivyo bali kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa awajibike katika hilo.”amesema .
Kaimu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum,Amon Mpanju amesema kuwa kwa Tanzania wameadhimisha siku hiyo November 22 2023 badala ya November 20 kutokana na muingiliano wa majukumu.
Aidha amesema serikali itahakikisha inasimamia haki za watoto dhidi ya ukatili wa aina yeyote ,kuendelezwa kielimu pamoja na kutobaguliwa na jamii.
Hata hivyo ili kutatua changamoto hiyo wazazi pamoja na watoto wanasema suala la mazingira liwepo katika mitaala ya elimu mashuleni ili kuwawezesha watoto hao kuwa na mbinu bora za kutunza mazingira pamoja na kuweka vipaumbele vyenye kulinda haki za watoto mashuleni na kwa jamii kwa ujumla.
Aidha Siku ya haki ya mtoto huadhimishwa ifikapo tarehe 22 mwezi Novemba kila mwaka ambapo mwaka 1959 baraza la umoja wa mataifa lilitoa tamko rasmi la kutambua haki za mtoto na kwa kuzingatia hilo taifa la Tanzania limeonekana kutelekeza kwa vitendo haki ya mtoto ikiwemo mtoto kupata elimu bure kuanzia awali hadi kidato cha sita.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo “mjengee mtoto uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yameandaliwa UNICEF ,Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum,pamoja na ofisi ya Rais Muungano na Mazingira .