Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Nov 22, 2023.
HALMASHAURI Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani, imeridhishwa na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Serikali mkoa ambao umetekelezwa kwa asilimia 98 :”;pamoja na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka trilioni 1.19 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Aidha imetoa rai kwa Serikali mkoa , kuhakikisha inaendelea kutekeleza kwa kasi miradi ya maendeleo ambayo bado haijakamilika ili ifikapo Disemba 2024 iwe imekamilika.
Hayo yalijiri wakati Kamisaa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) March 2021-Juni 2023, katika kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoani humo.
Kunenge alijinasibu kuwa wanatekeleza ilani kwa vitendo ,na kuahidi kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo ambayo ipo mbioni kukamilika .
Akielezea utekelezaji upande wa miundombinu alieleza ,ujenzi wa barabara kutoka Kibaha- Chalinze- Morogoro km 220 kuwa njia nne (Express way) mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa EPC +F Engineering, Procurement, Construction and Financing ,ujenzi unatekelezwa na Mwekezaji.
“Usanifu wa awali wa mradi huu kuanzia Kibaha hadi Morogoro umeshafanyika , kwasasa Mwekezaji anatafutwa ili ujenzi uanze”
“Barabara hii itapunguza changamoto ya msongamano wa magari na kupunguza ajali ambazo huwa ukijitokeza “alieleza Kunenge.
Hata hivyo Kamisaa huyo alieleza, miradi mingine inaendelea kwa kiwango cha lami katika barabara kuu na barabara za mkoa ikiwemo Kibaha – Mapinga km 23.
SEKTA YA VIWANDA
Idadi ya viwanda imeongezeka kutoka viwanda 1,472 mwaka 2022/2023 viwanda 120 ni vikubwa , 120 vya kati, 271 vidogo na 1,014 vidogo sana.
Kunenge alieleza, kunaongezeko la viwanda 53 ambavyo viwanda 30 ni vikubwa ,ujenzi wa viwanda vipya 15 vinaendelea.
UTALII
Utalii mkoa una vivutio 87 vinavyojumuisha mambokale, misitu ya Hifadhi ya mazingira asilia ,mapori ya akiba ya selous na Wamimbiki ,hifadhi za Taifa za Nyerere na Saadan na fukwe nzuri za bahari.
Ongezeko la watalii limepelekea mapato kuongezeka kutoka sh Bil 9,439,529,840 hadi sh.Bil 14,888,903,208.
Kunenge alieleza ,Mafia imejifungua na kujitangaza kwa utaliii wa Uchumi wa Bluu na Samaki papapotwe samaki anaevutia na kuwa kivutio kikubwa , na aliongeza wanaendelea kuutangaza mkoa kwa utalii uliopo.
NISHATI
Ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere JNHPP 2115 MV, utekelezaji umefikia asilimia 93 na unatarajia kukamilika Juni 2024.
Alieleza, njia ya kusafirisha Umeme ya 400 KV kutoka JNHPP hadi Chalinze 160 KV na usf 51 m,sh 39 Bilioni sawa na Jumla ya Bilioni 158 utekelezaji asilimia 99 ,utakamilika disemba 2023.
Kituo cha kupoozea umeme Chalinze Bilioni 128 utekelezaji umefikia asilimia 85.5 utakamilika disemba 2023.
MAJI
Mkoa una vijiji 417 ,mitaa 73 hadi sasa vijiji 331 vimepata maji yenye kujitosheleza, vijiji 57 vina huduma ya wastani sawa na asilimia 79.3 ya wakazi wote wa Mkoa ikiwa asilimia 77 ya wakazi wa Mkoa ikiwa asilimia 77 ya wakazi waishio Vijijini na asilimia 85 ya wananchi Vijijini.
AFYA
Kunenge alieleza, kuna ongezeko la upatikanaji wa dawa, vifaa tiba ,vitendanishi kutoka asilimia 92 kwa kipindi cha februari- machi 2021 hadi asilimia 93.2 kipindi cha april- mei 2023.
Tunaangalia bajeti inayoletwa kutatua changamoto,tunatekeleza , kuna miradi iliyokamilika ,na ipo ambayo haijakamilika,tunajinasibu tunatekeleza kwa vitendo na anayetaka kuyaona na kujifunza aje mkoa wa Pwani ajionee” alieleza Kunenge.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani, Mwinshehe Mlao alieleza , miradi imetekelezwa na amepongeza usimamizi mzuri unaofanywa kwenye miradi ya maendeleo.
Alitaka mkoa kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi ambayo inaendelea kutekelezwa .
Mlao alisema Chama na Serikali ni kitu kimoja ,hivyo alihimiza ushirikiano baina ya Chama na Serikali ili kuinua maendeleo na uchumi kwa wananchi.
Kwa upande wake ,Katibu wa CCM Mkoani Pwani, Bernard Gatty alieleza, kamati ya siasa ya mkoa ilifanya ziara katika wilaya zote kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama na kusema utekelezaji umefikia asilimia 98.
Alieleza kwa utekelezaji huo ,wanaimani na ushindi kwa uchaguzi ujao wa Serikali ya mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.
“Rais Samia Suluhu Hassan ametutendea haki kutuletea fedha nyingi, watalaam wamefanya kazi yao na Serikali kusimamia kikamilifu, hatuna shaka kujibu hoja kwa wapiga kura wetu,”alisisitiza Gatty.