Makamu wa pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla Akikata utepe kuashiria uzinduzi wa sera ya uchumi wa buluu na uvuvi katika hafla ya siku ya Uvuvi Duniani iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla akihutubia kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya siku ya Uvuvi Duniani hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Makame akizungumza machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais kuhutubia kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya siku ya uvuvi Duniani iliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Mhe .Hemed Suleiman Abdulla akipata maelezo kuhusiana na shughuli za Kampuni ya mwani kutoka kwa Kaimu Mkuu Idara ya fedha uwekezaji na masoko ZAFICO Mwanakheri Mohd hilali wakati alipotembelea maonesho ya uvuvi katika maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani yaliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mkuu Taasisi ya utafiti wa uvuvi na Maliasili za baharini Zanzibar Zakaria Ali khamis kuhusu kituo cha kutotolea vifaranga vya SAMAKI wakati alipotembelea maonesho ya uvuvi katika maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani. yaliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar
…….
Na Imani Mtumwa, Maelezo
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah khamis ulega amesema wataendelea kushirikiana vyema na Wizara ya uchumi wa buluu na Uvuvi katika kuhakikisha Uchumi wa Buluu unakuwa na kufikia asilimia 10 ya kuchangia pato la taifa ndani Nchini .
Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya Uvuvi Duniani huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege Waziri Ulega amesema mashirikiano yaliyopo kati ya Wizara hizo yamepelekea wavuvi kufanya kazi zao kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi.
Ameeleza kuwa katika kudumisha mashirikiano hayo wavuvi wa Zanzibar wanaruhusiwa kufanya shughuli za uvuvi Tanzania Bara kwa kutumia vibali hivyohivyo vilivyosajiliwa na Mamlaka husika za Zanzibar ili kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na kukuza pato la Taifa.
Aidha alisema Wizara hizo zitaendeleza programu za ugawaji wa maboti kwa wavuvi wadogo wadogo kwalengo la kuwainua wavuvi kiuchumi.
Awali alimshukuru Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaunga mkono kwa kutoa kipaumbele katika Sekta ya Uvuvi .
Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar DKT Aboud Suleiman Jumbe amesema Sekta ya Uvuvi inaendelea kutoa kipaombele kwa wanawake kwa kuwapatia vifaa mbali mbali vya uvuvi vikiwemo majaketi Maboti na Vifaa vya kuhifadhia samaki ili kuwaendeleza kiuchumi na kuwaepusha kuwa wa tegemezi.
Pia ameeleza kuwa dhana ya siku ya uvuvi Duniani ni kutokana na tamko la umoja wa mataifa kuhamasisha Uvui endelevu wenye tija kwa wananchi hivyo ni vyema kwa Wananchi kuachana na Uvuvi haramu sambamba na kuvitaka vyombo vya ulizi na usalama kuchukuwa hatua za kisheria ili kuondosha tatizo hilo.
Nao Baadhi ya Wavuvi mbali mbali walioshiriki katika maadhimisho hayo wamezishukuru Serekali zote mbili kwa kuwaunga mkono katika masuala ya Uvuvi kwa kuwapatia Vifaa mbalimbali vya Uvuvi na kuwajengea masoko ili kuweza kuuza samaki wao kwa uhakika na kwa usalama.
Katika Maadhimisho hayo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Hemed Suleima Abdallah alihutubia kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uvuvi Endelevu ni tija kwa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu “ na yamezinduliwa na akimuakilisha.