Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhawilishaji wa Teknolojia (CDTT) COSTECH Dkt. Gerald Kafuku wakati akifungua shindano la tafiti bora zaidi lilofanyika tarehe 20 Novemba, 2023 Kibaha, mkoani Pwani.
Dkt kafuku ameongeza kuwa Tafiti bora zaidi zitakazochaguliwa zitapelekwa sokoni kwaajili ya ubiasharishaji na kutatua changamoto zinazokabili jamii, mchakato wa kuwapata matokeo bunifu uliratibiwa mara baada ya COSTECH kutangaza kupitia Vyuo Vikuu ambavyo ni wanufaika wa Mradi wa mageuzi ya kiuchumi Elimu ya Juu maarufu kama ‘HEET’.
akifafanua lengo la kutenga fedha hizo ni kutoa nafasi kwa Vyuo Vikuu kushiriki mchakato huo ambapo jumla ya maombi ya tafiti 66 yalipokelewa na tafiti 22 zilipitia mchujo kupatikana 6, huku tafiti 5 zikitarajiwa kufuzu usahili huo.
Dkt. Kafuku ameongeza kuwa baada ya kupokea machapisho hayo Tume iliendesha Mafunzo ya siku tatu (3) ya kuandaa maandiko ya miradi yenye tija zaidi (proposals) ya kiuchumi na kijamii na kufanyia maboresho ili kuwezesha kuingia hatua nyingine ya mchujo baada ya uratibu wa sindano hilo, kwa lengo la kutoa hamasa kwa Vyuo Vikuu kutenga fedha za kugharamia matokeo ya Utafiti yatoke kwenye makabati na kuifikia Jamii ya watanzania.
Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi na Uhawilishaji na msimamizi wa programu ya Uendelezaji tafiti toka COSTECH, Dkt. Erasto Mlyuka alisema tunataka tafiti kwenye Taasisi za Elimu ya Juu zinufaishe jamii kwa kupitia hatua mbili (2) ikiwa ni ushiriki wa Vyuo Vikuu katika Mradi wa HEET kutathimini uwepo na matumizi ya Sera ya miliki dhihini ( _Institutional IP policy_ ) ili kujenga msingi uratibu wa kubiasharisha tafiti na bunifu ziweze kufikia viwango vya soko la Kimataifa.
Ameongeza pia, COSTECH imefanikisha miundombinu wezeshi ya kuunganisha Vyuo Vikuu na viwanda kuungana ili kuondoa dhana ya nadharia na kuwezesha mafunzo kwa vitendo kwa kusambaza Teknolojia na matokeo ya Utafiti na Ubunifu kwa jamii.