Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba akizungumza katika kikao kazi cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Novemba 21, 2023 katika Chuo cha Utalii (NCT) jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Thobias Makoba akitoa utangulizi wa kikaokazi hicho kilichofanyika kwenye Chuo cha Utalii cha Taifa NCT jijini Dar es Salaam.
Bw. Sabato Kosuri Afisa Mwansamizi wa Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina akitoa maelezo kadhaa kabla ya kuanza kwa kikaokazi hicho katika ya TEF. Ofisi ya Msajili wa Hazina na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USAF).
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Deodatus Balile akifafanua baadhi ya mambo yaliyojitokeza katika kikaokazi hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Thobias Makoba akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Deodatus Balile wakati kikaokazi hicho kikiendelea.
……………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na wadau wa Mawasiliano umefanikiwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa ajili kuhakikisha huduma ya mawasiliano inapatikana nchi nzima.
Akizungumza katika kikao kazi cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Novemba 21, 2023 katika Chuo cha Utalii (NCT) jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba, amesema kuwa katika fedha hizo serikali imetoa ruzuka ya shilingi bilioni 326.
Mashiba amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ambapo hadi sasa watanzania zaidi ya milioni 14 wanapata huduma ya Mawasiliano.
Amesema kuwa utekelezaji ujenzi wa minara unaendelea katika Kata 7,077 ili kufikia malengo tarajiwa.
Amefafanua kuwa mpaka sasa kuna minara 828 katika maeneo ya vijijini minara 1428 maeneo ya mjini.
“Wakati umefika wa kutumia huduma ya Tehama kwa ajili ya kujifunzia katika masuala mbalimbali ili kuleta tija” amesema Mashiba.
Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha huduma za mawasiliano inapatikana nchi nzima na kuleta tija kwa Taifa.
Mashiba amesema kuwa wamefanikiwa kutoa vifaa vya aina mbalimbali vya Tehama katika Shule 1,120 kwa ajili ya kujifunzia.