Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Salim Slim akizungumza na wahudumu wa Afya wa kujitolea (CHV) na Waandishi wa Habari wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na majanga ya dharura yaliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO na Kufanyika Zanzibar beach resort Mazizini.
Ofisa Uhusianao na uhamasishaji wa magonjwa ya mlipuko WHO Jaliath Rangi Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea juu ya kukabiliana na majanga ya dharurahuko Zanzibar Beach Resort
Mwasilishaji ambae pia ni Afisa kutoka WHO akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV juu ya kukakibiliana na majanga ya dharura yanapotikezea Hafla iliyofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Meneja wa Kitengo Cha Elimu ya Afya Zanzibar Bakari Hamad Magarawa akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV juu ya kukabiliana na majanga ya dharura huko Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya Waandishi wa Habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kukabiliana na majanga ya dharura yaliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO na Kufanyika Zanzibar beach Resort Mazizini.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la kiengereza la Daily news Issa Yussuf akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV kuweza kukabiliana na majanga ya dharura huko Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mhudumu wa Afya wa kujitolea shehia ya Pangawe Nadra Mussa Juma akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari na wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV kuweza kukabiliana na majanga ya dharura huko Zanzibar Beach Resort Mazizini. PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO
……
Na Sheha Haji Sheha, Maelezo
Wananchi wametakiwa kupuuzia taarifa za upotoshaji wa Majanga ya Kiafya zinazo sambazwa kwenye Mitandao ya kijamii ili kujihakikishia usalama wa afya zao.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya Zanzibar Dk. Salim Slim wakati akifungua Mafunzo ya Kukabiliana na Habari za upotoshaji wa Majanga ya afya huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Amesema kumekuwa na kawaida ya upotoshaji wa taarifa za Majanga ikiwemo miripuko ya Maradhi ya Matumbo na mengineyo katika Mitandao ya kijamii jambo ambalo huzusha taharuki kwa wanajamii.
Aidha, amesema mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika katika kuzusha upotoshaji wa taarifa jambo ambalo hutoa nafasi ya kuenea kwa haraka kwa upotoshaji huo kutokana na watu wengi kutumia mitandao hiyo.
Vile vile, amewaomba wananchi kuchukua tahadhari katika mvua za Vuli zinazoendelea kwa kufuata taratibu zote za kiafya ili kuepukana na Magonjwa ya Matumbo yanayoweza kusababishwa na Mvua hizo.
Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar Bakari Hamad Magarawa amewataka washiriki kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika majukumu yao ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa.
Mafunzo hayo ni ya siku moja ambayo yameandaliwa na shirika la Afya Duniani WHO na kuwashirikisha washiriki 110 wakiwemo Wahudumu wa afya wa kujitolea (CHV) pamoja na waandishi wa habari.