Adeladius Makwega-MWANZA
Asilimia 98 ya wanachuo wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya-Mwanza , wamefuzu vipimo vya vitendo uwanjani hapo wakati wakipimwa baada ya kuripoti chuoni hapo kwa masomo ngazi ya Astashahada na Stashahada mbalimbali za michezo kwa mwaka wa masomo 2023/ 2024.
Hayo yamesemwa na Mkufunzi Dennis Kayombo baada ya kufanyika kwa mazoezi hayo ya viungo na Utimamu wa Mwili Novemba 17, 2023 katika viunga vya chuo hicho chini ya usimamizi wakufunzi kadhaa wa chuo hiki cha umma.
“Hata hiyo asilimia mbili ya waliosalia inatokana tu hali ya kawaida, ikiwamo kubadilisha hali ya hewa, maana wanachuo hao wapo waliotoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na mataifa jirani.
Akizunguza huku akiendekea kusimamia mafunzo hayo, Mkufunzi Kayombo alisema kuwa hadi sasa wanachuo wageni waliopokelewa wanakaribia 150 ambapo idadi kama hiyo hiyo yaani wanachuo wanaoendelea na masomo kutoka mwaka wa masomo uliotangualia yaani 2022/ 2023 wao wameshaanaza masomo tangu Oktoba 2023.jumla kuu ikiwa wanachuo 300.Mkufunz kayombo aliongeza kuwa,
“Mazoezi ya utimamu wa afya yanasaidia kutambua afya zao, ilikutambua uwezo wa kufanya mazoezi, hata kama anashida hilo linatumika kutambua tu uwezo alionao na tunampa mazoezi kulinga na uwezo wake , hilo linafanyka baada ya kujaza fomu zao za afya Hosptalini wakiwa majumbani mwao kabla ya kuripoti.”
Mazoezi hayo ya mwanzo mwanzo yalimvutia mwandishi wa ripoti hii na hata alipojaribu kufanya hatua za awali alifuzu lakini mwisho ya mazoezi hayo alishindwa.