Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa tahadhari kwa wakazi wa Mkoa huo kuwa makini kipindi hiki cha mvua ambazo zinaendelea kunyesha ili kuepukana na majanga yanayoweza kujitokeza.
Akitoa taarifa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salvas Makweli leo Novemba 14, 2023 amesema kutokana na mvua hizo hadi sasa kwa Mkoa wa Arusha wamepokea taarifa za vifo vya watu Watano ambapo wanne tayari miili yao imetambuliwa lakini mmoja bado haujatambuliwa hivyo wananchi waliopotelewa na ndugu yao wameombwa kufika katika Hospitali ya Mount Meru kutambua mwili huo.
Sambamba na hilo pia wananchi wametakiwa kuwa makini hasa na watoto wadogo ambao wanahitaji uangalizi wa karibu, lakini pia kujiepusha kupita kwenye maji ya mito midogomidogo ama madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao hasa nyakati za usiku.