Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) James Andilile akimkabidhi moja ya jarida lenye ripoti maalum yenye utafiti wa huduma kwa wateja kwa Tanzania Bara wakati wa kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na Ofisi ya Masajili wa Hazina ambacho kimefanyika leo kwenye ofisi za EWURA barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) James Andilile akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na Ofisi ya Masajili wa Hazina ambacho kimefanyika leo kwenye ofisi za EWURA barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam kulia ni Titus Kaguo Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) James Andilile katikati akimsikiliza Titus Kaguo Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao kazi hicho.
……………………………….
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) James Andilile amesema serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya maji ili kuimarisha upatikanaji wa maji nchini
Hayo ameyasema leo novemba 6,2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na vyombo vya habari katika kikao kazi kilichoandaliwa na ofisi ya msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.
Amesema serikali imejiwekea mapango ya kuhakikisha ifikapo 2025 asilimia 95 ya watu wanaoishi mjini waweze kufikiwa na huduma ya maji safi na salama ambapo kijijini asilimia 85 na mpaka sasa mijini imefikiwa asilimia 88 huku vijijini ikiwa ni asilimia 77.
“Kwa mwaka jana miezi kama hii tulikua na mgogoro wa maji lakini serikali ikachukua hatua ikiwemo kuchimba visima virefu kwenye maeneo mbalimbali”amesemaAndilile
Amesema serikali ilichimba visima virefu kimbiji Bagamoyo vyenye thamani ya bilioni 46 na Mkuranga vyenye thamani ya bilioni 6 ili kuwezesha upatikanaji wa maji.
Aidha ameongeza kuwa ili kuongeza upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam kuna miradi mikubwa ambayo inaendelea ambayo ni bwawa la kidunda ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 10.
Amesema kufuatia visima vilivyochimbwa kimbiji na mkuranga vimepelekea kuwa na maji ya uhakika na kuondoa upungufu wa maji uliokuwepo awali.
Amesema miradi hiyo ya maji inatekelezwa kwenye majiji yote ikiwemo mwanza na Arusha.
Amesema katika jiji la Dodoma serikali imeshaanza kutekeleza mradi wa bwawa la Kwakwa lakini pia serikali inaendelea na utoaji wa maji ziwa Victoria na kupeleka Dodoma.
“Sisi kama mamlaka tunaendelea kufuatilia upatikanaji wa hudumua kupitia mamlaka za maji ambapo mpaka sasa tunazisimamia mamlaka 85 ili kuhakikisha huduma wanazotoa zinakua na ubora ma viwango vinavyostahili”amesema
Akizungumzia sekta ya umeme amesema serikali imeendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuhakikisha nchi inakua na umeme wa uhakika.
“Sasa hivi tuna mradi mkubwa wa Julius Nyerere Hidro Power Project ambao umekamilika kwa asilimia 9o ambao ukikamilika utaweza kuzalisha megawati 2515 lakini pia tunamradi wa Kinyerezi 1 ambao unazalisha megawati 185 lakini sasa hivi unazalisha megawati 180″ameongeza.
Amesema sambamba na hayo kuna mradi wa Rusumo ambao unazalisha megawati 87 ambazo zimefanywa kwa ushirikiano kati ya Burundi, na Tanzania na Rwanda ambapo mradi umekamilika kwa asilimia 99 sasa hivi nchi inapata megawati 26.7 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Amesema uwepo wa changamoto kwenye sekta ya umeme haimaanishi kama hakuna kinachofanyika.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Deodatus Balile kushoto nia Afisa Mawasiliano wa Ofisi ya Masajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea katika kikao kazi hicho.
Picha zikionesha baadhi ya wahariri wakiwa katika kikao kazi hicho.