Na. WAF, Dodoma
Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi ambapo ujenzi utaanza na jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD) ili litakapokamilika huduma zianze kutolewa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali Namba 78 kutoka kwa Mbunge wa Viti Malum, Mhe. Zainabu Athumani Katimba aliyeuliza ni lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa.
Dkt. Mollel amesema kuwa ujenzi huo utaanza mapema mwezi Januari 2024 ili wananchi wa Kanda ya Magharibi na mikoa jirani waweze kupata Huduma za afya kwa wakati.