Na Sophia Kingimali
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,
ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAZELA) na Jumuiya ya
Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) kupitia mradi wa kuinua
Wanawake na Uongozi, wameandaa tunzo maalum ya uandishi wa habari za
Takwimu za wanawake na uongozi ikiwa ni katika maadhimisho ya
kuelekea siku ya wanawake duniani
Kufuatia taarifa iliyotolewa kwa vyomba vya habari nchini imesema kuwa Tunzo hizo ni muendelezo wa shughuli zinazofanywa na mradi wa
kuinua wanawake na uongozi kufikia 50/50 katika ngazi zote
Aidha taarifa hiyo imesema kupitia
tasnia ya habari itawashajiisha waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari ikiwa na lengo la kutumia vyombo hivyo vya habari ili
kushajiisha masula ya wanawake na uongozi.
“jamii na Taifa
kwa ujumla wanapaswa kujua umuhimu wa wanawake kuwepo katika nafasi za uongozi ili
kukuza na kuimarisha demokrasia”imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Tunzo hii itahusisha kazi zilizotolewa katika vyombo vya habari vya aina
nne (4) ambavyo ni
Uandishi wa habari za Makala katika magazeti (feature articles)
Uandishi wa habari wa vipindi katika redio (radio program)
Uandishi wa habari katika Televisheni (TV program) na
Uandishi wa habari wa makala katika mitandao ya kijamii (feature articles in
social media story).
Hivyo, TAMWA ZNZ na washirika wake inawaalika waandishi wa habari
kukusanya kazi zao au kuandika katika eneo hilo na kuziwasilisha kwa wakati.
Imesema Kipindi cha Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe
katika ubora unaostahiki wakati
Kipindi au makala iliyochapishwa au kurushwa HEWANI katika vyombo
mbali mbali vya habari vikiwemo magazeti, runinga, redio na mitandao ya
kijamii katika kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2023.
Sambamba na hayo TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wake wametoa wito kwa wanahabari kujiendeleza zaidi katika fani lakini pia taasisi za habari pamoja na vyombo vya habari kuimarisha mafunzo ya muda
mfupi na muda mrefu kwa waandishi wa habari.
“Waandishi wa habari tufahamu kuwa kazi hii ni kusaidia jamii na hivyo ni
muhimu kutumia kalamu na vipaaza sauti katika kuelimisha na kuibua kero
na sauti za wasio na sauti”imesema sehemu ya taarifa hiyo
Amesema ni muhimu kwa waandishi na wahariri kuimarisha kada hii kwa kufuata kwa
vitendo maadili ya habari lakini wito kwa wahariri kuwasaidia waandishi
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hii ni mara ya tatu kufanyika tunzo ya aina hii ambapo mwaka jana 2022
jumla ya waandishi kumi walishinda tunzo za umahiri kwa upande wa
magazeti na mitandao ya jamii.
Kazi ziwasilishwe katika ofisi ya Chama cha ya Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) Tunguu karibu na IPA na
Kwa Pemba kazi ziwasilishwe katika ofisi ya Tamwa Chake chake Pemba.