Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Jamal Katundu akizungumza kwenye Mahafali ya 47 ya Chuo cha Maji ambayo yamefanyika Kwenye Ukumbi wa Mlimani City Leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa ngazi ya Cheti,Stashahada na Shahadabambao wamehitimu katika chuo Cha Maji wakiwa katika Mahafali ambayo yamefanyika Kwenye Ukumbi wa Mlimani City Leo jijini Dar es salaam.
..,……….,……
NA MUSSA KHALID
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Jamal Katundu amewasisitiza wakuu wa chuo cha Maji kuhakikisha wamasimamia misingi ya vituo katika kutoa mafunzo,kutoa ushauri elekezi pamoja na kufanya utafiti ili kuonyesha vyanzo vipya vya maji
Prof Katundu amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye Mahafali ya 47 ya Chuo cha Maji ambapo Jumla ya wahitimu 682 kuanzia ngazi ya Cheti,Stashahada na Shahada wamehitimu katika chuo hicho.
Aidha Profesa Katundu amesema ni vyema kukawekwa utaratibu wa vijana wanaohitimu wanapomaliza wakapatiwa mazingira wezeshi ambayo yataweza kusaidia katika ujasiriamali ili kuepukana na tatizo la ajira.
‘Tunachangamoto nyingi kwenye sekta ya maji ambazo zinahitaji utafiti na tunapoongelea chuo cha maji nchii ni hiki hivyo ni imani ya serikali kwamba tutaona sasa chuo likijikita katika utafiti ili kuleta suluhisho’amesema Prof Katundu
Pia Prof. Katundu amesema ukarabati na ujenzi wa miundombinu takribani 32 ya majengo ya utawala,Maktaba,Mabweni na Madarasa yanayogharimu shilingi bilioni 7.5 kutoka serikali kuu yatakamilika kwa wakati
Awali akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Maji,Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt Felician Komu amesema kuwa jukumu la chuo hicho ni pamoja na kutoa mafunzo yenye ubora kwa ajili ya kupata wataalamu sambamba na kufanya utafiti katika masuala mbalimbali.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho, Japhet Jeremia pamoja na Fatma Iddi wamesema lengo la kusoma kozi hiyo ni kwenda kuisaidia jamii katika utatuzi wa changamoto za maji.
Hata hivyo wahitimu hao wametakiwa kujifunza kuihudumia nchini yao lakini pia kushiriki katika fursa mbalimbali kwa kutengeneza miradi na kuanzisha kampuni na serikali itakuwa tayari kuwasaidia.