……….
Katika kuhakikisha miradi ya maendele ya Serikali inatekelezwa kikamilifu na kwa wakati kama lilivyo lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Judith Nguli na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mvomero Watembelea Chuo Kikuu Mzumbe.
Ziara hii imefanyika Novemba 02, 2023 ikiwa na lengo la kukagua mradi ya Serikali inayotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe, Mradi huo ni ujenzi wa Hosteli za kisasa eneo la Maekani Chuo Kikuu Mzumbe.
Awali akizungumza baada ya kumpokea Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkrugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Sophia Joseph Mchomvu, kwa niaba ya Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha. Bi. Sophia amemkaribisha Chuoni hapo na kumueleza hatua ambazo zinaendelea kutekelezwa na ambazo tayari zimeshakamilika kwani baadhi ya Hosteli zimekamilika na zimeshaanza kutumika.
Aidha Bi. Sophia Mchomvu alitoa nafasi Kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Miliki Bw. Wolta Shiyo na timu yake walioambatana pamoja wakati wa kutembelea, kutoa maelezo na kuona mradi huo na hatua zilizofikiwa.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Judith amefurahishwa na hatua za utekelezaji wa mradi huo na amesisitiza watendaji kuendelea kusimamia vizuri na kwa weledi mkubwa shughuli zinazoendelea.
Mheshimiwa Judith ametumia nafasi hiyo pia kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma katika taasisi za elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe. Hii ni heshima kubwa kwa Chuo, Wilaya, Mkoa na hata Taifa kwani Chuo Kikuu Mzumbe kinatoa huduma nchi nzima.
Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, Tujifunze Kwa Maendeleo ya Watu”