Na WMJJWM Dodoma
Serikali imeziagiza Taasisi za umma na binafsi kuweka mpango maalum wa kuwapa kipaumbele wazee kwenye huduma wanazotoa ili kupunguza changamoto zinazo wakabili.
Hayo yamesemwa Bungeni Novemba 02, 2023 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis kufuatia swali la swali la Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mhe. Michael Constantine Mwakama aliyetaka kujua ni limi Serikali itawasilisha Maswada wa Sheria ya wazee Bungeni.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema Serikali inathamini mchango wa wazee na kuwaenzi kwa kuweka mifumo rafiki itakayo wahakikisha wawezesha wazee kupata huduma za msingi kulingana na mahitaji yao.
Ameongeza kwamba Sera ya Wazee ya mwaka 2003 ipo katika hatua ya mwisho ya maboresho yake, hivyo tamati la zoezi hilo itarahisisha kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria hiyo Bungeni
“Serikali yetu imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha Wazee wanapata huduma za kijamii bila vikwazo vyovyote, hivyo Taasisi za Umma na Bifasi zingatieni huduma bora kwa wazee” amesema Naibu Waziri Mwanaidi.
Akijibu swali la Mhe. Juliana Didas Masaburu Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua Serikali itakipandisha lini hadhi Chuo cha Mandeleo ya Jamii Buhare Musoma kutoa elimu ngazi ya shahada, Mhe. Naibu Waziri Mwanaidi amesema Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutathimini utoaji wa kozi hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira, kwani ili Chuo kitoe elimu ngazi ya Shahada kinatakiwa kuwa na vigezo ikiwemo kupata ithibati kamili, kuwa na miundombinu ya kukidhi utoaji wa elimu hiyo, rasilimali za kutosha na kukidhi vigezo husika.
Aidha amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum, itaendelea kuboresha miundombinu kwenye Vyuo vya Mandeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara kwakutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ili kupunguza changamoto za malazi kwa wanafunzi hao.
Naibu Waziri Mwanaidi amewahakikisha wabunge kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mikoa kuhakikisha inakuwa na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii katika maeneo yao ili kutoa fursa kwa vijana kusoma fani hiyo itakayo wawezesha kutatua changamoto jamii.