Bariki Masawe Meneja wa Mauzo na Usambazaji Kampuni ya Bia Tanzania TBL Kanda ya Mashariki akizungumza mara banda ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye hoteli ya Double View Sinza jijini Dar ea Salaam.
Bariki Masawe Meneja wa Mauzo na Usambazaji Kampuni ya Bia Tanzania TBL Kanda ya Mashariki akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo hiyo yaliyofanyika kwenye hoteli ya Double View Sinza jijini Dar ea Salaam.
……………………….
Jumla ya wanufaika 100 wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wamehitimu mafunzo ya kukuza biashara zao yaliyotolewa na TBL.
Mafunzo hayo pia yamelenga kuwapa uzoefu na mbinu bora zaidi za kukuza biashara zao.
Wiki iliyopita TBL ilianza safari ya kuwainua na kuwawezesha wauzaji rejareja chini ya mpango unaojulikana kwa jina la Mpango wa Maendeleo ya Rejareja (RDP), uliozinduliwa jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2023.
Mpango wa Kukuza Wafanyabiashara, chini ya kauli mbiu GRIT (Kukua Kiuvumbuzi Pamoja), ni mpango ambao unatazamiwa kuwasaidia wauzaji rejareja kukuza biashara zao na kujifunza ujuzi mpya.
Mpango huu unalenga kuongeza ukuaji, elimu, na kujumuika kwa kuwafunza wauzaji rejareja juu ya mada kadhaa, ambayo ni pamoja na usimamizi wa fedha, usimamizi wa bidhaa , Masoko na mauzo, na uuzaji unaozingatia misingi ya biashara.
Mafunzo ya biashara yaliyolengwa yatawezeshwa na wataalam wa sekta, na wauzaji waliochaguliwa kwa awamu ya majaribio ya mpango huu watapitishwa katika moduli tano za mtaala wa ujuzi sambamba na miongozo ya wawezeshaji na vitabu vya washiriki vyenye mahitaji ya wauzaji wa rejareja yaliyotambuliwa kwa kuzingatia mambo muhimu ya kufanikisha mabadiliko.
TBL ina zaidi ya wauzaji rejareja 26,000 kote nchini. Mpango wa maendeleo ya wauzaji rejareja ambao utatekelezwa kwa awamu, unahakikisha kuwa wafanyabiashara hao wanajifunza mbinu mpya za biashara na kuweza kuendelea kustahimili mabadiliko ya mazingira ya biashara, ambayo yanaendelea kutatizwa na mabadiliko ya kidijitali.Kwa hivyo, ujumuishaji wa teknolojia ya dijiti ni moja ya zana muhimu ambazo wauzaji watajifunza.
Kama mlipakodi mkubwa Tanzania, TBL pia ni miongoni mwa waajiri wakuu nchini, huku maelfu ya watu wakitoa bidhaa na huduma moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kampuni hiyo ya bia katika mnyororo wake wa usambazaji.
Jose D. Moran, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, alisema kuwa programu ya maendeleo ya wauzaji rejareja ni sehemu ya dhamira ya TBL katika kuleta matokeo chanya katika jamii ya Kitanzania. “Siku zote tunajitahidi kuwa na athari chanya katika jamii yetu na tumejitolea kwa mtazamo wa ukuaji unaozingatia watu. Mpango huu wa maendeleo ni dhihirisho la dhamira hiyo.”
Meneja miradi endelevu wa TBL, Siya Mbuya, alisema mpango huo unatoa ujuzi muhimu kwa wauzaji rejareja ambao wengi wao ni tegemezi katika familia zao. “Tumeamua kuzindua upya mpango wa maendeleo ya wauzaji rejareja kama sehemu ya juhudi zetu pana za kuwezesha jamii. Wauzaji wote waliochaguliwa watajifunza mbinu endelevu za biashara na ujuzi ambao utawasaidia kukua.”
Mkufunzi wa programu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Dotto Paul Kuhenga , alisema GRIT inawahimiza wauzaji rejareja kufikiria upya mifumo ya zamani ya uendeshaji.
“Tunawahimiza wauzaji wa rejareja kuwa wabunifu na wepesi zaidi katika uwezo wao wa kuwahudumia wateja na wapinzani wao wa kibiashara.”
Mpango wa mafunzo hayo unaanza Oktoba 24, 2023 jijini Dar es Salaam na kumalizika Oktoba 31, 2023.