Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na MichezoMhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na wasanii wakati akizindua tuzo za kimataifa za muziki (Zanzibar international Music award) ,Huko Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo za kimataifa za muziki (Zanzibar international Music award) Ramadhan Bukini akitoa maelezo mafupi kuhusiana na tuzo hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Taifa (BASATA ) Dk.Kedmon Mapana akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na MichezoMhe.Tabia Maulid kuzindua za tuzo za kimataifa za muziki ,hafla iliyofanyika Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na MichezoMhe.Tabia Maulid Mwita akicheza,kutunza na kufurahi pamoja na wasanii wa ngoma ya kibati wakati wa uzinduzi wa tuzo za kimataifa za muziki ,Huko Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa tuzo ya kimataifa ya muziki (Zanzibar international Music award) uliofanyika Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na MichezoMhe.Tabia Maulid Mwita akionesha mfano wa tuzo ya kimataifa ya muziki mara baada ya kuizindua huko Madinatul Al Bahr Mbweni Zanzibar.
…………….
Na Mwashungi Tahir, Maelezo
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe,Tabia Maulid Mwita amesema Serikali ina mpango wa kujenga chuo cha Sanaa kitakacho wawezesha wasanii kujiendeleza na kuzalisha kazi zinazoendana na soko la sanaa la kimataifa.
Akizungumza katika uzinduzi wa tuzo ya kimataifa ya muziki (Zanzibar international Music Award ) huko Madinatul Albahr Waziri Tabia amesema hatua hiyo ni pamoja na kuimarisha miundombinu itakayowezesha wasanii kuzalisha kazi zao katika mazingira mazuri.
Ameongeza kuwa kwa sasa wasanii wanafanyakazi katika mazingira magumu jambo linalosababisha kutofikia malengo yao .
Akitaja utaratibu wa ugawaji wa tunzo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya kimataifa ya muziki (Zanzibar international Music award) Ramadhan Bukini amesema Tasnia ya muziki imekua kwa kasi hivyo ni lazima kwa wasanii kufanya muziki unaoendana na soko la kibiashara.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema kuanzishwa kwa tunzo hiyo kutasaidia wasanii kupata fursa ya kutangaza kazi zao na kujulikana kimataifa.
Nao wasanii wamesema wamefurahishwa na hatua ya Serikali ya kuweka tunzo kwani zitasaidia kujitangaza na kufika mbali.