Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi wa Synergy Tanzania Altaf Mansoor ameipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa madini nchini ili kukuza na kuendeleza sekta hiyo.
Hayo ameyasema leo Oktoba 25, 2023 ,jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini 2023 wakati alipotembelea kwenye mabanda mbalimbali yalipo kwenye mkutano huo.
Amesema hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara ya madini kukutana na kujadili changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo kwa maslahi mapana ya nchi.
“Serikali imetusaidia kutuletea fursa hii tunapaswa kuitumia kama ukiona peke yako uwezi tunaweza kuungana tukafanya biashara kubwa yenye tija na maslahi makubwa kwetu kama wafanyabiashara lakini pia nchi”amesema Mansoor
Aidha ameongeza kuwa ukuaji wa sekta ya madini unachangia ongezeko la uchumi kwani ajira nyingi zinazalishwa na ulipaji wa kodi unaongezeka hali inayosaidia upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule,hospitali na miundombinu ya barabara.
Sambamba na hayo nasoor amesema kuwa ili kufanikisha shughuli za madini wafanyabiashara wanapaswa kushirikiana.
Amesema watanzania wanapaswa kutumia hizi fursa ili waweze kuwekeza kwani hata kama kwa kuungana lakini si kuziacha.
“Utendaji wa serikali unategea kwa kiasi kikubwa kodi zetu hivyo tunapaswa kuchangamkia fursa ambazo zitasaidia kuongeza ulipaji wa kodi”amesema.