Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Jenifa Christian Omolo akionesha moja ya jarida linaloelezea kuhusu uchumi wa Tanzania wakati akifungua kongamano la wahariri wa vyombo vya habari na wakuu wa vitengo vya mawasiliano na masoko wa taasisi zilizo chini ya wizara ya fedha lenye lengo la kujengeana uwelewa kwenye masuala la habari, masoko na mawasiliano linalofanyika mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Jenifa Christian Omolo akionesha moja ya jarida linaloelezea kuhusu uchumi wa Tanzania wakati akizungumza wakati akifungua kongamano la wahariri wa vyombo vya habari na wakuu wa vitengo vya mawasiliano na masoko wa taasisi zilizo chini ya wizara ya fedha lenye lengo la kujengeana uwelewa kwenye masuala la habari, masoko na mawasiliano linalofanyika mjini Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny Mwaipaja akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo ili kufungua kongamano la kongamano la wahariri wa vyombo vya habari na wakuu wa vitengo vya mawasiliano na masoko wa taasisi zilizo chini ya wizara ya fedha lenye lengo la kujengeana uwelewa kwenye masuala la habari, masoko na mawasiliano.
…………………………….
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Jenifa Christian Omolo amewataka wadau wa habari kuandika habari zenye mashiko kwa taifa ili kuitangaza nchi lakini pia kulinda amani umoja na mshikamoano uliopo.
Hayo ameyasema leo Oktoba 25, 2023 mjini Morogoro wakati akifungua kongamano la wahariri wa vyombo vya habari na wakuu wa vitengo vya mawasiliano na masoko wa taasisi zilizo chini ya wizara ya fedha lenye lengo la kujengeana uwelewa kwenye masuala la habari, masoko na mawasiliano.
Amesema waandishi wanapaswa kuandika taarifa ambazo zitaitangaza taarifa na vivutio mbalimbali vilivyopo ili kuitangaza nchi na kuvutia uwekezaji.
“Waandishi wa habari ni watu muhimu kwani taarifa zinazotolewa na nyinyi zinaaminika na zinasomwa sehemu kubwa ndani na nje hivyo ni vizuri kutumia fursa hiyo kuandika mambo mazur ya taasisi zetu ambayo yanayojenga nchi”amesema Omolo.
Ameongeza kuwa mawasiliano ndio msingi wa mafanikio ya taasisi na nchi hivyo yanapaswa kutumika vizuri kwa maslahi mapana ya nchi.
Amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanakwenda pia vijijini na kuandika habari ambazo zitaibua changamoto katika mambo ya kijinsia na kijamii ambazo zitasaidia taifa kusonga mbele katika maendeleo na kusaidia watu wenye changamoto mbalimbali kujikwamua kutoka katika hali mbaya waliyokuwa nayo na kuwa na hali nzuri.
“Dunia ni Kijiji cha Digital Marketing hivyo kama Maafisa Mawasiniano na Masoko katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha mna wajibu wa kutumia fursa hiyo ili kutangaza mambo mema ambayo wizara na taasisis zake inafanya jambo ambalo litasaidia kuiweka nchi katika ramani znuri duniani katika masuala mbalimbali ikiwemo uchumi,” Amesema Jenifa Omolo.
Richard Kayombo Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akifafanua jambo kuhusu shughuli mbalimbali za TRA katika kongamano hilo linalofanyika mkoani Morogoro.
Karimu Meshack Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano NIC Insurance akizungumzia mafanikio na maboresho waliyoyapata kama taasisi ya bima ya serikali.
Picha mbalimbali zikiowaonesha maafisa mawasiliano na masoko wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa vyombo vya habari wakishiriki katika kongamano hilo linalofanyika mkoani Morogoro.