Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Zephania Sumaye amefungua rasmi huduma kwa wagonjwa wa nje (OP) katika Kituo cha Afya Kiegeani ,ambapo kinakuwa ni mkombozi kwa wananchi kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kiafya .
Akifungua huduma hiyo, Sumaye ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali wananchi wake, hasa katika sekta ya afya kwa kuboresha upatikanaji wa huduma.
Aidha, amewataka viongozi na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kukamilisha kwa wakati mradi kwa sehemu zilizobaki ili wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.
Kituo cha Afya cha Kiegeani kimegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni moja na kinatarajiwa kuondoa kero kwa wananchi wa kata ya Kiegeani kwa kuepuka kwenda umbali mrefu kufuata huduma.