Na Prisca Libaga Maelezo Arusha
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Tanzania inakwenda kunuifaka kwa kuingiza kiasi cha dola za Marekani Milion 7.7 sawa fedha za Tanzania shilingi Bilion 18. katika kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoanza kesho Ijumaa Oktoba 20 na kuendelea hadi Novemba 9 Mwaka huu Jijini Arusha.
Akieleza maandalizi ya kikao hicho kikubwa barani Afrika, Balozi Dk, Pindi Chana ameeleza kikao hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Serikali ya Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho ni cha siku 20 kikifamyika katika kumbi Mbalimbali zilizopo katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Arusha(AICC) kikijikita katika masuala ya mtambuka ya haki za binadamu kwa nchi za Afrika
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC Ephraim Mafuru amesema mpaka sasa jumla ya washiriki 919 kutoka nje ya nchi na 400 wa hapa nchi wameshawasili Jijini Arusha kwa ajili ya mkutano huo.