Picha ya pamoja kati ya waandishi wa habari na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa akifungua semina na ziara kwa Waandishi wahabari juu ya shughuli na kazi zinazofanywa na JICA.
Mshauri Mwandamizi wa JICA Tanzania Raymond Msoffe akiwasilisha taarifa yake juu ya miradi ya JICA mbele ya Waandishi wa habari.
Afisa utawala na Mawasiliano JICA Tanzania, Alfred Zacharia akiongoza semina hiyo iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Mshauri wa Uchumi
baina ya Japani na Tanzania Christopher Ntaigiri akitoa wasilisho lake mbele ya Waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiendelea kusikiliza ma wasilisho yalitolewa kwenye semina hiyo iliyofanyika mkoani Kilimanjaro
(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY)
*********
Na James Salvatory
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini ili kuwajengea uelewa juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo.
Mafunzo Hayo ya siku tatu, yalienda sambamba na ziara katika miradi inayotekelezwa JICA katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Akifungua Mafunzo hayo Mkoani Kilimanjaro, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa amesema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari kufahamu kwa kina shughuli mbalimbali za JICA na Ubalozi wa Japani nchini Tanzania na kuujulisha umma kwa usahihi.
Katika ziara hiyo, waandishi wa habari wametembelea mradi wa ujenzi wa shule katika shule ya msingi kibohehe wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, mradi wa kuimarisha mpango wa Maendeleo ya kilimo ya wilaya na uwezo wa utekelezaji kwa kutumia mbinu ya SHEP(TANSHEP) na mpango wa JICA wa kujitolea ambao Malengo yake ni kushiriki katika Maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ujenzi wa nchini zinazoendelea.
Mradi mwingine ni Arusha-Holili Road, KAISER mradi ambao huboresha uwezo wa uzalishaji viwandani na mradi wa kusafirisha umeme kati ya Tanzania na Kenya (KTPIP) kwa msongo wa kilovoti 400.
Katika hatua nyingine Balozi Yasushi Misawa amewataka watanzania kuwa watu wa kuzingatia muda wakati wakifanya majukumu yao ya kila siku ili kuokoa muda unaoweza kupotea pasipo sababu za msingi Hali ambayo inachangia kurudisha nyuma uchumi wa nchini.
“Huwa nashangaa rafiki zangu wa kitanzania wakipoteza muda hata hawakasiriki kabisa na hawajali jambo ambalo kwa kwetu Japan tunazingatia muda ” alisema Balozi
Kwa upande wake Mshauri Mwandamizi wa JICA Tanzania, Raymond Msoffe, amesema uwepo wa miradi ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan litasaidia kuboresha mahusiano ya kijamii na kiutamaduni.
Naye Mshauri wa Uchumi baina ya Japani na Tanzania Christopher Ntaigiri akizungumzia juu ya kumbukizi ya ya miaka 30 ya TICAD na miaka 10 ya ABE Initiative.
“Kongamano la Kimataifa la Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD) hufanyika Mara moja kila baada ya miaka mitatu ambapo huzungumzia kuboresha ushirikiano baina ya Afrika na Japani” Alisema Ntaigiri.