Mbozi-Songwe.
Mahakama ya wilaya ya Mbozi imemtia hatiani na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 Gerezani mshitakiwa Willison Kibona (36) kwa kulima Bangi.
Kibona alikamatwa 26 Desemba, 2022 nyumbani kwake Ihanda akiwa na miche ya Bangi 335 yenye uzito wa kilo 13.8 ambayo aliipanda kwenye nyumba yake. Akitoa hukumu hiyo Oktoba 17, 2023
Mheshimiwa Nemes Chami amesema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mshtaka na kumtia hatiani mtuhumiwa. Mshtakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili kukomesha ulimaji wa Bangi.