Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama nchini humo, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) (wa pili kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama nchini humo wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akisalimiana na Bw. Lucas Malaki ambaye ni mmoja wa vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania (hawapo pichani ) ambao wamerejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo, nyuma yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima walipofika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akimsikiliza kijana Lucas Malaki aliyerejea nchini kutoka Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo |
…………………………….
Watanzania 9 waliokuwa nchini Israel wamerejea nyumbani leo tarehe 18 Oktoba 2023 na kulakiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mapokezi ya Watanzania hao Naibu Waziri Byabato amesema kurejea nyumbani kwa Watanzania hao kunatokana na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko nchini Israel ili waendelee kuwa salama.
Amesema Serikali kupitia Ubalozi wake wa nchini Israel iliweka utaratibu wa kuwarejesha Watanzania wote ambao wangetaka kurudi nyumbani na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuwashawishi Watanzania walioko nchini humo ili waone haja ya kurudi nyumbani hadi pale hali itakapotengemaa.
Amesema Serikali imefarijika kwa Watanzania hao kuitikia wito wa kuokoa maisha yao na anaamini kuwa Watanzania waliobaki nchini humo busara zao zitawaongoza na kuamua kurejea nyumbani ili wawe salama na kuongeza kuwa Serikali itawarejesha nyumbani watakapokuwa tayari kufanya hivyo.
Akizungumza baada ya mapokezi hayo mmoja wa Watanzania hao Bw. Lucas Malaki ameishukuru Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha nyumbani na kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya wajisikie fahari kuwa watanzania na kuwaondolea unyonge na kuongeza kuwa wanakichukulia kitendo hicho kuwa ni cha upendo na cha kizalendo na kuahidi kuwa wataendelea kuwa raia wema.
Watanzania hao wamerejeshwa nyumbani na Serikali kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya amani na usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani tangu kikundi cha HAMAS kilipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba, 2023.