Nzega Vijijni-Tabora
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji katika Kata ya Puge Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora.
Waziri wa Maji (Mb), Mhe. Jumaa Hamidu Aweso amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Wizara yake italeta Fedha hizo mapema iwezekanavyo ili kuwaondolea tatizo la maji wakazi wa Kata ya Puge.
Serikali inapeleka Fedha hizo za mradi wa maji Kata ya Puge kufuatia Ombi la Mbunge wa Nzega Vijijini Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala ambaye amesema ni kata moja tu ya Puge katika Jimbo lake ndio yenye changamoto ya uhaba wa maji.
Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoani humo.
Takwimu za Hali ya Maji Nzega Vijijini;
Jumla ya Vijiji ni 141
Kata zote zimefikiwa na Maji bado 1
– Bajeti ya mwaka huu ni Tsh 10,356,254,930.00
– Idadi ya miradi iliyokamilika kuanzia 2021 Hadi sasa ni 16, idadi ya wanufaika ni 56,608 yenye jumla ya DPs ni 112 na Gharama ya Tsh. 9,358,894,910.79
– Miradi inayoendelea ni 10 yenye wanufaika 40,126 na DPs 80 kwa gharama ya Tsh. 7,593,407,397.99