Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais) Menejimenti ya utusmishi wa Umma na Utawa;a Bora, George Simbachawene akizungumza na mlengwa wa TASAF, Mwanauani Mohammed katika kijiji cha Bamba wilayani Mkinga, Tanga, JUmanne Oktoba 17,2023. Bi Mwanauani, anayejishughulisha na uzalishaji wa mwani ni mmoja wa akinamama walioonesha bidhaa zao wakati Simbachawene alipotembelea walengwa wa TASAF katika kijiji hicho
…………………………
WAZIRI wa Nchi (Ofisi ya Rais) Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawla Bora, George Simbachawene amefafanua utaratibu wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa kushiriki kazi za ajira za muda.
Akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF wilayani Mkinga mkoani Tanga Jumanne Oktoba 17, 2023 Waziri Simbachawene amesema ni muhimu kwa wanufaika na watekelezaji wa mradi mdogo wa Ajira za Muda kuzingatia masharti ya kushiriki katika shughuli hizo.
Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais) Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene akizungumza na mlengwa wa TASAF, Mwanauani Mohamme ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mwani kutokana na manufaa anayopata kutokana na ruzuku za TASAF. Mwanauani ni mmoja wa akinamama kadhaa walilioonesha bidhaa zao kwa Waziri walipowatembelea katika kijiji cha Bamba
Ameyataja masharti hayo kuwa ni mshiriki kuwa na umri kati ya miaka 18 na 65, kutokuwa na hali ya ulemavu na kutokuwa mjamzito au mwenye mtoto mdogo.
Amesema katika siku za karibuni kumekuwa kukitokea sintofahamu kutokana na watu kutoelewa masharti ya kushiriki katika shughuli hizo.
Simbachawene ametembelea barabara iliyojengwa kwa nguvu za walengwa katika mradi wa Ajira za Muda.
“Sio lengo kuwafanya mlime barabara kwa mikono, bali ni kuwapeni ajira za muda na kuwafanya mjifunze kujitegemea,” amesema.
Akizungumzia malalamiko kuwa watu wasio na sifa wanaingizwa kwenye Mpango wakati wenye sifa wanaachwa, amesema kuwa kama hilo lipo basi ni makosa ya watendaji vijijini kwa kuwa walengwa hapo kuchaguliwa na wananchi wenyewe katika Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Amewataka wananchi kuwa makini kila inapotokea fursa ya utambuzi wa Kaya za kujngia kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.