Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Dkt.Paul Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
………
Julieth Laizer, Arusha.
Majaji Wakuu 16 wanatarajia kukutana katika mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF),ambao watajadili kuzingatia utawala wa sheria,demokrasia na uhuru wa mahakama.
Aidha wataelimishana na kubadilishana uzoefu wa utatuzi wa changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma ya utoaji wa haki kwa wananchi.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Jaji wa Mahakama ya Rufani,Dk Paul Kihwelo, wakati akizungumzia maandalizi ya mkutano huo,katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Arusha.
Amesema katika kubadilishana uzoefu wa utatuzi wa changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma ya utoaji wa haki kwa wananchi majaji hao watakutana kwa siku nne kuanzia Oktoba 23,2023 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Amesema majaji hao watatoka nchi za Angola, Botswana, Eswatin, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zanzibar, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Amesema Majaji Wakuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika katika kutambua jukumu muhimu la Mahakama ndani ya Kanda, waliamua kuanzisha Jukwaa la Majaji Wakuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika mwaka 2003.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Profesa Elisante Ole Gabriel,amesema tangu kuundwa kwa jukwaa jilo tangu kuundwa kwake limeleta mafanikio mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo,kukuza mahusiano baina ya nchi na nchi pamoja na diplomasia ya uchumi kuzidi kujua.