Na Sophia Kingimali,
Gari aina ya scania lenye usajili wa namba T124 ECX linalobeba sumu ya Sodium Cyanide inayapeleka Migodini mitatu nchini limepata ajali eneo la Kagongwa na sumu hiyo kumwagika.
Akizungumza leo Oktoba 17 Wilaya ya Kahama baada ya kufika kwenye tukio Kamanda wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Janeth Magomi amesema alipata taarifa majira ya saa 3:20 asubuhi gari la Kampuni ya Taifa Transport & Logistic limedondoka katika Kata ya Kagongwa Wilaya ya hiyo kwenda eneo tukio.
Amesema vyombo vya usalama vinaendelea na udhibiti kuepusha madhara kwa wananchi lazima tahadhari ziwepo kwa sababu sumu ni hatari.
“Nilivyofika kwenye eneo la tukio ni kweli ajali imetokeoa na huduma za uokaji zinaendelea ambapo dereva mmoja kati ya madereva kumi waliokuwa wakisafirisha sumu ya Sodium Cyanide amepata ajali na kapewa huduma na kuhakikisha madhara hayotokei kwa wananchi, ” amesema Kamanda Magomi.
Amesema dereva huyo amepewa huduma ya kwanza kutoka kwa waaguzi na anaendelea vizuri.
Amesema amewasisitiza wananchi waendelee kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wanaopoona matukio ya aina hiyo na hawasogei eneo hilo kwa tahadhari hadi sasa hakuna madhara yeyote.
Aidha amesema hali ni shwari kawato wasi wasi wananchi wote wa eneo hilo na kuwataka waaendelee na shughuli zao za kila siku na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Naye, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mkaguzi wa Wilaya ya Kahama, Edward Selemani amesema wao wamejianda kufanya uokaji muda wowote tukio linapotokea.
Amesema walivyopokea taarifa za tukio hilo walijiaanda kwa kuvaa vifaa vya uokozi na kuhakikisha sumu ya Sodium Cyanide isilete madhara kwa wananchi.
“Wananchi wanapaswa kuwa na tahadhari kubwa matukio kama haya yanapotokea na wasigelee eneo hili kwa sababu sumu ni hatari na unaweza kupoteza maisha,”amesema Selemani.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa Mtaa wa Kashime, amesema walipata mshituko kuona tukio la ajali hiyo.
“Ajali hii imetuogopesha tumepata taharuki maana gari limeandikwa hatari na sumu tuona dereva anadondoka baada ya muda tukaona watu wanaangaika na kutoa huduma ya kwanza ikabidi tukae mbali na eneo hili ,”amesema Mabula.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Taifa Transport &Logistic, Happiness Nyiti amesema amepokea taarifa za ajali akiwa kwenye Mgodi wa Buzwagi na ilimbidi afike kwenye eneo la tukio.
“Ni kweli ajali iliyotokea ni gari ya kampuni yetu gari aina ya scania lenye usajili wa namba T124 ECX linalobeba sumu aina ya sodium cyanide inayopelekwa kwenye migodi ya Buzwagi, Bulyankulu na North Mara,”amesema Nyiti.
Amesema kwanza anashukuru vyombo vya usalama na wadau kwa kuweza kudhibiti ajali hiyo hadi sasa hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa wananchi na hali ya dereva anaendelea vizuri kwa sasa.
Aidha ameongeza kuwa wanafanya mafunzo ya mara kwa mara ya madereva wote wanaoendesha magari yanayobeba sumu ya sodium cyanide.
“Mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kupewa vyeti kwaajili ya kusafirisha sumu ya Sodium Cyanide na tunahakikisha wakiwa safarini madereva wana vifaa vya kujikinga na sumu hizo ikiwepo mbele Convoy Leader na Escot,”ameongeza.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:00 asubuhi ambayo ilizua taharuki kubwa kwa wananchi wa eneo hilo wakipewa tahadhari wasisogee eneo la tukio kuna hatari wakae mbali ili kuepusha madhara ajali hiyo hajasababisha kifo wala majeruhi ambapo ajali ilitokea wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga.