Wakat Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ameshaingia mkoani Tabora kwa ajili ya ziara ya kikazi, wakazi wa Kata ya Ziba wilayani Igunga, wamemuhakikishia Rais Samia ulinzi wa kura zake ndani ya mkoa wa Tabora.
Wakazi hao wa Ziba wamemuhakikishia Rais Samia ulinzi huo kwa kutumia silaha za jadi, ambapo ilibidi wakusanyike na kufanya matembezi maalum ya pamoja kwa ajili ya kumpokea kabla ya hajafika kuzungumza nao.