Kaimu Mkurigenzi wa Benki ya TIB akizungumzia malengo ya Benki hiyo na mikakati yake wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali katika kikaokazi katika ya Ofisi ya Madajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kilichofanyika kwenye jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam Leo Oktoba 16, 2023.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya TIB Lilian Mbassy katikati pamoja na baadhi ya viongozi wa Benki hiyo wakiandika mambo muhimu wakati wa kikaokazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF jijini Dar es salaam, kulia ni Kwenye kiting wa TEF Deodatus Balile.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano. Kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri akifafanua baadhi ya mambo wakati kikaokazi hicho kiliendelea.
…………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Kaimu Mkurugenzi Benki ya Maendeleo (TIB), Bi Lilian Mbassy amewataka wadau mbalimbali wa kilimo nchini kuchangamkia fursa ya kupata mkopo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo na kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza leo Oktoba 16, 2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika kwenye Jengo la Golden Jubile jijini Dar es Salaam Bi. Mbassy amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa riba ya gharama nafuu kuanzia asilimia nne hadi tano.
Amesema kuwa wadau wa kilimo wanapata fursa ya kukopa kuanzia shilingi milioni 50 hadi bilioni moja kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Bi. Mbassy amesema kuwa TIB inatekeleza majukumu yake kwa kujiwekea mikakati na kutekeleza kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano pamoja mpango mkuu wa uendelezaji wa sekta ya fedha.
Amesema kuwa wataendelea kufanya kazi na benki kuu ya dunia kupitia mradi wa upanuzi wa umeme vijijini kwa kutoa mikopo kwa wazalishaji katika utekelezaji.
“Tayari tumefanya kazi baadhi ya mikoa na sasa tunaendelea katika mikoa mengine kupitia kwa wadau wanaozalisja umeme” amesema
Amesema kuwa wanatengemea kuendelea kufanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Amesema kuwa kuna miradi mengi ambayo inatarajia kuanza Utekelezaji kuanzia mwaka 2014 ikiwemo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Ameeleza kuwa wapo katika mipango ya utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa meli chini ya huduma za meli, uwekezaji katika upanuzi viwanda vya Sukari ikiwemo Kagera Sugar pamoja na Mtibwa Sugar pamoja na upanuzi wa Bandari kavu.
Amefafanua kuwa wanaendelea na juhudi za wanaunga mkono sera ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini yenye kuleta tija kwa Taifa.