Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limetangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha kivutio bora cha utalii barani Africa (African leading tourist Attractions) na kupewa tuzo na mtandao wa _World travel awards_.
Tuzo hiyo imetolewa usiku huu wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya _Atlantis The Royal Dubai _ katika nchi za Falme za Kiarabu ambapo Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kushinda vivutio vingine vya utalii barani Afrika ambavyo ni table Mountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya afrika kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramis of Giza ya Misri.
Tuzo hiyo imepokelewa na Meneja wa huduma za Utalii NCAA Bw. Peter Makutian kwa niaba ya uongozi wa Shirika.