Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MAOFISA TEHAMA nchini, wameaswa kwenda na wakati ,kupenda kujifunza kulingana na teknolojia inavyobadilika ili kujiongezea uzoefu na ujuzi.
Aidha wawe wabunifu ,wajitume ili kuacha alama na tija katika kada hiyo kwenye maeneo ya kazi
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani Rashid Mchatta, wakati alipomwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, kufungua kikao kazi cha mwaka 2023 ,ambacho kimefanyika Kibaha Mkoani Pwani na kukutanisha maofisa hao kutoka mikoa mbalimbali nchini ili kujadili changamoto zinazokikabili kitengo Cha TEHAMA.
“IT ina mambo mengi sana, inabadilika kama mtu wa Tehama hufanyi updating itakupa wakati mgumu,
“Someni masomo ya ziada kuongeza uzoefu,mkoa wa Pwani ndio mwenyeji mwaka huu tumejipanga kuhakikisha tuliyoyajadili yanafanikiwa”anasema Mchatta.
Mchatta alieleza, kada ya TEHAMA imekua kwa kasi kubwa na kupelekea kuwa mhimili mkubwa katika utendaji kazi na Serikali na Taasisi nyingine binafsi kwenye mifumo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za mitaa ,mfumo wa kusimamia huduma za hospitali.
“Serikali – TAMISEMI imeipa kada hii umuhimu mkubwa kwa kuanzisha wizara rasmi inayoshughulikia TEHAMA ,hivyo tusimuangushe mh Rais”
Awali Melchiory Baltazary, Mkurugenzi Msaidizi-TEHAMA TAMISEMI alieleza kikao hicho ni kikao kazi ambacho kitafanyika siku mbili.