Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuabukizwa Dkt. Sarah Maongezi, wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati wa kusoma tamko la Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katika kuelekea wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza maadhimisho yake yatafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodom kuanzia Novemba 9 hadi 14 mwaka 2019.
Dkt.James Kiologwe,akifafanua jambo kuhusu Ugonjwa wa Kisukali na Shinikizo la juu la Damuya kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mapema kabla ya kusomwa kwa tamko la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati wa kusoma tamko la Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katika kuelekea wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza maadhimisho yake yatafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodom kuanzia Novemba 9 hadi 14 mwaka 2019.
Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuabukizwa Dkt. Sarah Maongezi akiwasilisha mada juu ya Ugonjwa wa Saratani kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mapema kabla ya kusomwa kwa tamko la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati wa kusoma tamko la Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katika kuelekea wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza maadhimisho yake yatafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodom kuanzia Novemba 9 hadi 14 mwaka 2019.
…………….
Na Alex Sonna
Wakazi wa Dodoma na mikoa jirani wametakiwa kujitokeza kupima afya zao katika wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayofanyika Novemba 9-14, mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma katika tamko la Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu lililosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuabukizwa Dkt. Sarah Maongezi kuhusu wiki hiyo.
Amesema katika wiki hiyo wananchi watapimwa afya zao na kupata ushauri wa kitaalam juu ya afya zao.
“Tumeamua kufanya maadhimisho haya kutokana na kuwepo na changamoto kubwa katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kila mwananchi atakaye jitokeza ndani ya siku za maadhimisho haya ataweza kupatiwa vipimo vya afya na ushauri wa kitaalam kuhusu afya yake,”amesema.
Ameeleza kuwa kubadilika kwa mtindo wa maisha kumekuwa kukisababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta madhara.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema kauli biu ya maadhimisho hayo ni “Tutembee pamoja katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoabukiza” kwa lengo la kutaka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali yao hususani sekta ya afya katika kumalisha afya za watanzania ili kuweza kufikia kuleta maendeleo kwa taifa tukiwa na afya zilizo imara.
Amesema inahimiza ushirikiano katika kudhibiti magonjwa hayo kwani mapambano dhidi ya vihatarishi vya magonjwa yasiyoambukiza yanahusisha mshikamano wa sekta mbalimbali, wadau, mtu mmoja mmoja na wananchi kwa ujumla.
Mkuu huyo amesema wiki hiyo itazinduliwa Novemba 9 na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
Amesema lengo ni kuhimiza wananchi kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kwa jamii.
Magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa, magonjwa ya figo, seli mundu, magonjwa ya akili, magonjwa ya macho, kinywa pua, koo na masikio,ajali na matatizo yanayorekebishika kwa utengamao.