Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu amefanya ziara na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme unaotokana na Umeme wa joto ardhi kilichopo kijiji cha Mbeye 1 kata ya Isongole.
Katika ziara hii Mhe Haniu ameagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huu kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia upatikanaji wa nishati hiyo kwa wakati
Aidha ameagiza kuendelea kuajiri vijana wanaopatikana katika mazingira yanayozunguka mradi huu ili kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.
Kituo hiki kilichopo ndani ya Msitu wa Ziwa Ngosi kinatarajia kuzalisha kiasi cha Megawati 70 mara kitakapokamilika.
Umeme huu unaozalishwa kwa kutumia mvuke uliopo chini ya ardhi unatarajia kuleta manufaa lukuki ikiwemo kuigizwa katika grid ya taifa na hivyo kupanua upatikanaji wa umeme nchini, Pamoja na kupatikana joto asilia litakalotumika kukaushia mazao kama chai, pareto, Kakao, kahawa na mengine mengi.
Hivyo mradi huu unaenda kuondoa adha ya ukataji miti ovyo kwa ajili ya upatikanaji wa nishati hasa katika viwanda vya ukaushaji wa mali mbichi.