Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola (kulia) akiwa na Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Bw. Stephen Maganga (kushoto) akifafanua jambo katika Operesheni ya ukaguzi miundombinu ya umeme Kata ya Kisarawe II, Wilaya Kigamboni uliyofanyika leo Oktoba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola akizungumza na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa miundombinu ya umeme Kata ya Kisarawe II, Wilaya Kigamboni leo Oktoba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Bw. Stephen Maganga akizungumza na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa miundombinu ya umeme Kata ya Kisarawe II, Wilaya Kigamboni leo Oktoba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wakazi wa Kigamboni kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola akizungumza na Wakazi wa Kigamboni kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme.
Baadhi ya picha zikionesha uharibifu wa miundombinu ya umeme ikiwemo wizi wa mashine umbo (Transformer) ambao umefanywa na watu wasiojulikana katika Kata ya Kisarawe II, Kigamboni, Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiwa katika Operesheni ya ukaguzi miundombinu ya umeme Kata ya Kisarawe II, Wilaya Kigamboni uliyofanyika leo Oktoba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke kupitia Operesheni ya ukaguzi wa miundombinu amebaini uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umeme ikiwemo wizi wa mashine umba (Transformer) katika Kata ya Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni.
Akizungumza leo Oktoba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam akiwa Operesheni ya ukaguzi miundombinu ya umeme katika Kata ya Kisarawe II, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola, amesema kuwa kuna maeneo 10 katika Wilaya ya Kigamboni ambayo yamefanyiwa uharibifu wa mashine umba (transformer).
Mhandisi Mashola amesema kuwa uharibifu huo umefanywa na watu wasiojulikana katika Kata ya Kisarawe II ambao umeusababishia hasara shirika takribani shillingi milioni 40.
Amesema kuwa uharibifu huo umesababisha wateja zaidi ya 200 kukosa huduma ya umeme, jamii kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali pamoja na shirika la TANESCO kukosa mapato kutokana na wizi wa mashine umba (transformer)
“Watu wasiojulikana wameiba mashine umba (transformer, wameshusha chini na kutoa wire aina ya copper kimepelekea wateja kukosa huduma ya umeme” amesema Mhandisi Mashola.
Amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na jitihada za kusambaza umeme, lakini wapo baadhi ya watu wanahujumu miundombinu ya TANESCO.
“Transformer imeibiwa sasa inabidi tuleta nyingine mpya ambayo ingeweza kutusaidia kupeleka sehemu nyengine ili watanzania waweze kupata huduma ya umeme” amesema Mhandisi Mashola.
Ametoa rai kwa wananchi kuwa na jukumu la kulinda miundombinu ya TANESCO la kila mtu, huku akisisitiza kuwa “ukiona mtu anachimba chini katika miundombinu ya TANESCO kwa ajili ya kutoa Copper toa taarifa kwa uongozi wa serikali za mtaa ili tuweza kumkamata mtu na kumchukulia hatua za kisheria”
Mhandisi Mashola ameeleza kuwa Operesheni hiyo ni endelevu na sehemu ya majukumu yao ya kila siku katika kuhakikisha wanakagua miundombinu pamoja na kutatua changamoto za wateja.
Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Bw. Stephen Maganga, amesema kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa mali za shirika kutokana zinamilikiwa na watanzania kwa asilimia mia moja.
Bw. Maganga amesema kuwa tunapoendelea kulinda miundombinu ya TANESCO kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo ambalo linaleta tija kwa maendeleo ya Taifa.
Amesema kuwa sheria ipo wazi endapo mtu akibainika amefanya kosa la kuiba miundombinu ya TANESCO anakuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Bw. Maganga ameeleza kuwa kuwa hivi karibuni TANESCO wamepata ushindi wa kasi moja ya uhujumu uchumi namba 5, 2022 ambapo mtuhumiwa mmoja mahakama imemuhukumu kwenda jela miaka 20 kwa jela kwa kosa la kuiba miundombinu ya shirika.
“Mtuhumiwa huyo aliingia katika miundombinu ya TANESCO na kukata kipande cha wire cha mita 156 ambayo ni kesi tulipata ushindi na alihukumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi” amesema Bw. Maganga.
Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile, amewataka wananchi kutimiza uwajibu wao wa kulinda miundombinu ya TANESCO ili kuhakikisha wanapata huduma ya umeme muda wote.
“Sisi kama wananchi tuna uwajibu wa kuhakikisha tunalinda miundombinu, tunapodai haki na nyinyi mtimize uwajibu wenu, uhalibifu huu unafanya na ndugu zetu, jamaa zetu ni watu ambao wapo katika jamii yetu na kusababisha sisi kukosa huduma ya umeme” amesema Dkt. Ndugulile.
Hata hivyo wakazi wa Kata ya Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni wameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke kuweka uzio katika maeneo yote yenye mashine umba (transformer) ili kuimarisha ulinzi.
“Katika maeneo ambayo yamejificha TANESCO wanapaswa kuweka kuzio ili mtu asifanye uharibifu wowote katika transformer kutokana sisi wananchi tunapata hasara kubwa kutokana na kukosa huduma ya umeme” amesema Sophia Juma.