Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Peter Kumalilwa akitoa maelezo mafupi leo kabla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(wa pili kutoka kushoto) .
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akitoa maelezo mafupi leo kuhusu kampeni ya kuboresha miundombinu ya elimu kabla ya kupokea mifuko 100 ya saruji kutoka Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena.
Bwana shamba na Mauzo wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Khaji Halidi akitoa maelezo leo kuhusu matumizi ya mbolea za aina mbalimbali wakati walipokabidhi mbolea za kukuzia miti kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala( mwenye shati nyeupe)
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (kushoto) akipokea msaada mifuko ya saruji 100 kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Peter Kumalilwa (kulia) kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Tabora.
……………………………………………………
KAMPUNI ya Petrobena East Ltd imetoa mifuko 100 ya saruji na mifuko 10 ya mbolea katika Manispaa ya Tabora ikiwa ni kuunga mkono juhudi Serikali za ujenzi wa madarasa na utunzaji wa mazingira.
Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Peter Kumalilwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala.
Alisema kuwa Kampuni hiyo imefurahishwa na juhudi za Serikali za kuboresha elimu nchini zinazoendelea na hivyo wameamua kushiriki katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia.
Kumalilwa alisema kuwa sanjari na utoaji wa saruji hiyo wameamua kutoa mbolea mifuko 10 kwa ajili ya kukuzia miti ambayo imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora ili kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala alisema kuwa msaada huo utasaidia kuunga mkono jitihada zao za kuboresha miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Tabora kwa ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu ikiwemo kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.
Alisema mifuko 50 itakwenda kata ya Uyui na iliyobaki 50 itapelekwa Kata ya Ifucha ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Kitwala alisema wako katika kampeni ya kuhakikisha kuwa inaondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kutembea umbali mrefu kutoka kwao hadi shule , jambo linalodhofisha ufaulu wa wanafunzi.
Aidha alisema kuwa pia wanampango wa kujenga Sekondari katika Kata ya Ifucha ambayo haina Sekondari.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ifucha Juma Abdallah aliishukuru Serikali kwa hatua ya kuamua sehemu ya msaada uliotolewa na Petrobena kusaidia wananchi wa eneo hilo ili kuongeza vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi.
Aliongeza kuwa tayari wananchi wa endeo hilo wamekusanya vifaa mbalimbali kama vile mchanga na mawe wakisubiri kuungwa mkono ili nao waweze kujenga Sekondari yao ya Kata kwa ajili ya kuondolea adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wanasoma Sekondari katika Kata jirani.
Naye Said Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Petrobena kwa kutoa msaada huo ambao sehemu ya mifuko hiyo itasaidia kujenga vyumba vya madarasa katika Shule shikizi.
Alisema shule shikizi zinasaidia kupunguza tatizo la watoto kutembea umbali mrefu kutafuta haki yao ya kupata elimu.
Aidha Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena kwa kuamua kushughulikia tatizo la zao la tumbaku ikiwemo usambazaji wa mbolea mapema.