Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia Kitengo cha Makosa dhidi ya Mtandao leo Oktoba 10, 2023 katika shule ya sekondari Vwawa limetoa elimu ya makosa dhidi ya Mtandao kupitia kwa Mkuu wa Makosa ya Mtandao mkoa wa Songwe D/Cpl Magere Chacha.
D/Cpl Magere amewafundisha wanafunzi wa shule hiyo maana ya makosa ya mtandao na hasara zake, sheria zinazo simamia makosa ya mtandao na adhabu zake ikiwa ni pamoja na madhala ya ushoga, usagaji na mmomonyoko wa maadili kupitia mitando na kujifunza tamaduni za nje kama vile aina ya uvaaji na mabadiliko ya mfumo mzima wa maisha ya kila siku.
Aidha ameongeza kwa kusema kupitia mitandao watu wanakumbana na ukatili kama vile kusambaza picha za utupu kwa watoto au kuwaonesha watoto picha za utupu na video ngono.
“Tambueni Vijana ni nguvu kazi ya leo inatakiwa kutokufanya matendo hayo ili waweze kutimiza malengo katika masomo yao” DCpl Magere ameyasema hayo.
Sambamba na hayo amewataka wanafunzi na walimu kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ila kupunguza uhalifu katika maeneo yao.