Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Godfrey Chongolo, akishiriki Kikao cha Shina. Namba 03, Kipundu, Nkasi, Mkoa wa Rukwa, alipowasili mahali hapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuhamasisha uhai wa CCM kwenye ngazi ya mashina, kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia majawabu na kukagua miradi ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025.