NA NOEL RUKANUGA
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wamefanikiwa kuibuka na ushindi ugenini wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo Oktoba 8, 2023 katika Uwanja wa Liti Mkoani Singida.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti umesoma Singida Big Stars 1-2 Simba.
Bao la Saido Ntibanzokoza dakika ya 26 lilikuwa la mipango na bao la pili la Moses Phiri lilikuwa ni pigo kubwa kwa Singida Big Stars baada mpira kumshinda Beno Kakolanya.
Bao la Singida Big Stars lilifungwa na Deus Kaseke kutokana na makosa ya Ally Salim katika kuokoa hatari.
Simba Sc inaongoza Ligi ikiwa na Pointi 15 ikiwa baada ya kucheza mechi tano msimu wa 2023/24.
Bingwa mtetezi Yanga naye alipata matokeo ugenini katika mchezo uliopita baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold.