Na Sophia Kingimali
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELLA)wamesema wataendelea kuwafikia
Kwa kuwafuata wateja wake kwenye maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wanawasaidi kusajili na kuuisha taarifa za taasisi na kampuni.
Akizungumza kwenye maonesho ya swahili tourism Expo 2023 afisa leseni Koyan Aboubakar amesema katika maonyesho hayo wamefanikiwa kusajiri wateja wapya zaidi ya 50.
“Ushiriki wetu kwenye maonyesho haya ya utalii ili kuwasaidia hawa wenye makampuni ya utalii amabao hawajasajiri au kuhuisha taarifa zao pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kusajili kampuni zao”amesema Aboubakar
Amesema biashara ya utalii imekua sana nchini hivyo wanaojihusisha na biashara hiyo ni vyema kujisajiri ili kuwa na leseni zao za biashara.
Amesema tangu kuanza maonesho hayo oktoba 6 mpka leo Oktoba 8 wameweza kutatua changamoto mbalimbali za wateja.
“Changamoto kubwa tunayokutana ni elimu ya jinsi ya kutumia mtandao kwenye kujisajili na kuhuisha taarifa zao hapa kwa muda wa siku hizi tatu tumeshasaidia watu zaidi ya 50.amesema Aboubakar.