Wakala wa vipimo mkoani Njombe umeendesha operesheni ya ukaguzi wa mizani ya kupima uzito katika hospitali ya rufaa Kibena, vituo vya afya pamoja na zahanati mkoani humo na kubaini kuwa idadi kubwa ya mizani inayotumika inadosari hatua ambayo inahatarisha afya za wagonjwa ambao wapo kwenye hatari ya kuzidishiwa ama kupunguziwa dozi ambazo zinatolewa kulingana na uzito wa mgonjwa.
Zoezi hilo limefanyika ikiwa dunia ina adhimisha wiki ya vipimo duniani ambapo mara baada ya kufanya operesheni hiyo meneja wa wakala wa vipimo mkoani humo Gasper Matiku ametoa wito kwa uongozi wa vituo hivyo vya afya pamoja na hospitali ya rufaa kuhakikisha wanarekebisha mapema mizani hiyo ili kunusuru afya za wagonjwa wanaoweza kuingia hatarini kwa kupewa dozi kimakosa.
Clouds Tv imezungumza na kaimu mganga mkuu wa hospitali ya rufaa kibena Barnaba Mgonja pamoja na Shela Myemba muuguzi msaidizi katika kituo cha afya njombe mjini wanazungumzia athari za kutumia mizani mibovu katika kutoa huduma za afya .
Katika mizani 26 ambayo imekaguliwa 14 imegundulika kuwa na dosari kiasi ambacho ni sawa na asilimia 38 ya mizani yote iliyokaguliwa .