NA
K-VIS BLOG, MBEYA
MAADHIMISHO
ya wiki ya Huduma kwa Wateja yamefikia kilele leo Oktoba 6, 2023 ambapo Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini, wametumia maadhimisho hayo kwa kujumuika pamoja watumishi na wateja (wanachama)
na kisha wateja kupewa zawadi ya miche wakapande na kuitunza.
Kimsingi
wiki ya Huduma kwa Wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa
huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano
kwa watoa huduma na wateja.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inatamka “Ushirikiano kwa Huduma Bora.”
ikilenga kuhamasisha ushirikiano baina ya watumishi (watoa huduma) wenyewe,
lakini pia ushirikiano na wateja ili hatimaye kila upande ufurahie HUDUMA
BORA.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, aliwaongoza watumishi wa Mfuko huo
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, yenye makao yake makuu jijini Mbeya, kutoa
huduma kwa wateja sanjari na kuwapatia zawadi za miche, ikiwa ni sehemu ya
kampeni ya Mfuko wa PSSSF, kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza
na wateja (wanachama) wa PSSSF waliofika kwenye ofisi za PSSSF jijini humo, ili
kupata huduma, Bw. Kijazi alisema, Mfuko unawathamini sana na katika maboresho
makubwa ya utoaji huduma, mtumishi anayekaribia kustaafu sasa atawasilisha
madai kupitia mtandao.
Pia,
PSSSF imewarahisishia wastaafu wake kujihakiki kupitia simu janja (Smart
phones).
“Mstaafu
akishajihakiki kwa alama za vidole (biometric) hatalazimika tena kuja ofisini
kujihakiki, na badala yake atatumia simu janja (smart phone)
kujihakiki akiwa mahala popote.” Alifafanua Bw. Kijazi.
Miongoni
mwa huduma ambazo Bw. Kijazi alishirikiana na watumishi kuwahudumia wateja (wanachama)
ni pamoja na huduma za Uhakiki, huduma za taarifa za michango, lakini pia
kusikilzia changamoto kutoka kwa wateja na kupokea maoni kwa nia ya kuboresha
zaidi utoaji huduma.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jijini
Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week)
Oktoba 6, 2023.
Meneja
wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhan Mgaya (kulia), akimkabidhi
zawadi ya mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa PSSSF kwenye ofisi za Kanda
jijini Mbeya, Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu wa Mfuko wa Pensheni PSSSF Paul Kijazi, (kulia) akimkabidhi
mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa Mfuko huo, Kanda Nyanda za Juu Kusini,
kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika ofisi za Kanda zilizopo
Jijini Mbeya.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (wapili kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jijini
Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week)
Oktoba 6, 2023.