Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Grace Musita akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati ilipotembelea miradi ya Shirika la Nyumba la NHC ya Morocco Square na Samia Scheme Kawe ili kupata uzoefu Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati ilipotembelea miradi ya Shirika la Nyumba la NHC ya Morocco Square na Samia Scheme Kawe ili kupata uzoefu Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah kulia akiongozana na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati ilipotembelea miradi ya Shirika la Nyumba la NHC ya Morocco Square na Samia Scheme Kawe ili kupata uzoefu Oktoba 6, 2023.
Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Grace Musita akitoa maelezo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Zanzibar Mhe. Juma Makungu Juma katikati na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati ilipotembelea miradi ya Shirika la Nyumba la NHC ya Morocco Square na Samia Scheme Kawe ili kupata uzoefu Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah kulia akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati ilipotembelea miradi ya Shirika la Nyumba la NHC ya Morocco Square na Samia Scheme Kawe ili kupata uzoefu Oktoba 6, 2023.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Zanzibar Mhe. Juma Makungu Juma amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kutekeleza miradi kwa ufanisi ambayo inaleta tija kwa Taifa katika kufikia malengo.
Akizungumza Oktoba 6, 2023 wakati akiongoza kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ziara ya kutembelea miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa Morocco Square na Samia Scheme Kawe Jijini Dar es Salaam, Mhe. Juma, amesema kuwa NHC wamepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi.
“Tumejifunza namna wanavyopata faida kupitia miradi, wapangaji wa bara wana utayari wa kulipa kodi tofauti na Zanzibar wamekuwa wakisuasua” amesema Mhe. Juma.
Mhe. Juma amesema kuwa Zanzibar wanategemea kufanya makubwa kwani tayari wamesaini makubaliano ya ushirikiano na NHC katika kufanikisha utekelezaji wa miradi Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah, amesema kuwa ujio wa kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni muendelelezo wa ushirikiano ambao tayari walisaini miezi mitatu iliyopita Jijini Dodoma.
Bw. Abdallah amesema kuwa wataendelea kutekeleza maagizo ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo wamekuwa wakisisitiza ushirikiano ili maendeleo yaliyokuwa upande mmoja yafanyike kwa upande mwengine kupitia njia ya kujifunza.
“Leo kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamekuja kuangalia kazi zetu, wito wangu kwa taasisi nyengine tuwe na ushirikiano wa pande zote mbili kwani kuna kitu cha kujifunza, pia tushikane mkono pale ambapo unaona mwezanko ana kitu na unaweza kujifunza” amesema Bw. Abdallah.
Amesema kuwa pia timu ya wataalamu kutoka Shirika la Nyumba Zanzibar wanatarajia kuja kujifunza kwa NHC, huku akibainisha kuwa wanatarajia kwenda Zanzibar kwa lengo la kuangalia wanafanya nini ili waweze kujifunza pamoja na kufanya majadiliano yenye lengo kusaidia katika kuhakikisha wanapinga hatua kila mmoja.